Radi yaua mmoja aliyekua amejihifadhi kwenye mti akijikinga na Mvua
Na Ibrahim Yassin,Chunya
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Gilagwenda dadii (27) mkazi wa kitongoji cha Itumpi kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kupigwa na radi.
Akizungumza leo 28/ Novemba 2024 ndugu wa marehemu huyo Rashid Samwel amesema ilikua saa 10 jioni ndugu yake alienda kutengeneza baiskeli kwa fundi alikutwa na umauti baada ya kupigwa na radi.
Amesema akiwa chini ya mti uliokaribu na fundi huyo mvua ilianza kunyesha kwa kasi takribani dakika 30 ilikuja radi iliyosababisha umeme ukatike kwa muda na kusababisha kifo hicho.
Amesema baada ya kifo hicho watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kata walisogea na nilipo mpekuwa mfukoni nilimkuta na pesa 50.000 na vidonge vya kutuliza maumivu kwani alikuwa ana fanya vibarua kuweka marudio kwenye Planti.
Afisa mtendaji wa kata ya Matundasi Salu Ngele alisema yeye sio msemaji wa tukio hilo hivyo hawezi kuzungumza chochote licha ya kuwepo eneo la zahanati ulipopelekwa mwili huo.
Diwani wa kata ya Matundasi Timo Choga licha ya kudhibitisha uwepo wa tukio hilo, amesema limetokana na radi huku akiwataka wananchi kutokaa chini ya miti ya asili nyakati za mvua.
"" ni kweli tumekumbwa na tukio hilo ni mpango wa mungu ila natoa rai kwa wananchi kuacha kuk aa chini ya miti ya asili nyakati hizi za mvua na pia tuhakikishe mashimo yote yanafukiwa. kuhepuka maafa" amesema Choga.
Amesema licha ya radi hiyo kuua pia ataendelea kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha mashimo yana fukiwa ili kuhepuka maafa nyakati hizi za mvua za masika zinazotarajia kuanza msimu huu.



Comments
Post a Comment