UMOJA WA WANAWAKE SOKO LA DHAHABU CHUNYA WATOA MISAADA KWA YATIMA.
Na Ibrahim Yassin, Chunya
UMOJA wa Wanawake (Chunya Queens) katika soko la madini ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya, wametoa misaada ya vitu mbalimbali vikiwemo vyakula vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 2 kwa watoto yatima.
Akizungumza jana na Dirakamilifu, mwenyekiti wa umoja huo Jelroline Charles amesema wao ni wafanyakazi wanawake katika soko la ununuzi wa madini, wameanzisha umoja huo kwa ajili ya kusaidiana.
Amesema licha ya kusaidiana kwenye shida na raha pia wameweka ajenda ya kusaidia yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu .
Amesema hivi juzi tu walienda kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Itua jijini Mbeya ambapo walitoa mchele, unga, sukari, mafuta, sabuni na Pedi zikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 2.
Amesema baada ya kutoa vitu hivyo pia waliweza kula nao chakula pamoja ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo watoto hao ambao wengi wao ni walemavu wa viungo.
Nae katibu wa kikundi hicho Dolla Gibson amesema lengo kuu la umoja huo ni kusaidiana kwenye misiba na sherehe lakini wameweka kipengele hicho cha kusaidia yatima na kitakuwa endelevu.
Amesema mbali na kutoa misaada kwa yatima pia wameweza kumchangia fedha mtoto aliyetak iwa kufanyiwa upasuaji hospitali ya Ikonda baada ya mama yake kutokuwa na uwezo na wamefaniki sha hilo.
Amesema katika maeneo mengi wapo watu wenye uhitaji hivyo aliomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kwani wapo wanao tupa vyakula na wa po wenye nguo nyingi hazivaliwi wanatakiwa kuw apatia watu wenye uhitaji.
" suala.hilo litakuwa endelevu na siku chache zijazo tutakuwa na tulio la utoaji wa misaada katika vituo vingine vya yatima na tutaendelea kufanya hivyo kuunga mkono jitihada za Serikali" amesema Gibson.




Comments
Post a Comment