Madereva halmashauri Nkasi wapewa somo kuyatunza magari na kufuata kanuni za kazi
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 ya mwaka huu Halmashauri ya wilaya Nkasi imekarabati magari yote yaliyokua yameharibika huku madereva wakipewa somo namna ya kuyatunza magari hayo Ili yaweze kudumu Kwa muda mrefu.
Akizungumza na Madereva hao afisa usafirishaji wa Halmashauri ya wilaya Nkasi Rashid Hand Masud amewataka Madereva hao kufuata kanuni za kazi yao ya udereva Kwa kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kuendesha Kwa ustadi huku wakiongozwa na kanuni za Utumishi wa Umma.
Amesema dereva yeyote ambaye ataonekana kuendesha magari hayo kinyume na utaratibu unaowaongoza atanyang'anywa gari na kukabidhiwa mtu ambaye atakua na uwezo wa kuyaendesha magari hayo Kwa kufuata misingi ya kazi na kanuni za Utumishi wa Umma.
Amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa wilaya Afraha Hassan Kwa uamuzi wake wa kuyafufua magari yote yaliyokua yameharibika kiasi kwamba Kwa Sasa Kila dereva ana gari lakini pia itarahisisha shughuli za Halmashauri kwenda Kwa haraka kutokana na kuwa kuwa na magari mengi.
Madereva Kwa upande wao wamemshukuru mkurugenzi mtendaji Kwa kuweza kuyakarabati magari hayo kitu ambacho kimewawezesha wao kutoka kijiweni na kuwa kazi ya kufanya baada ya magari yao kuwa barabarani.
Wamedai kuwa Kwa Sasa wao watajitahidi kuyatunza magari hayo kadiri wawezavyo na kuwa watazingatia kutoa taarifa za haraka hasa pale gari inapohitaji huduma kabla ya gari kuharibika kabisa na kuwa Kwa kufanya hivyo magari hayo yatadumu Kwa muda mrefu.

Comments
Post a Comment