Wanunuzi wa dhahabu Chunya waomba kuwekewa huduma za kibenki kurahisisha kazi zao



Na Ibrahim Yassin ,Chunya

WANUNUZI wa madini ya dhahabu katika soko la.madini wilayani Chunya mkoani Mbeya, wameiomba serikali kupitia wizara ya madini kuweka huduma za kibenki katika soko hilo ili kurahisisha ufanyaji kazi.

Akizungumza jana na DiraKamilifu Msafiri Miraji amesema soko hilo ni kubwa na lina wanunuzi hai 52 hivyo waliomba vyumba vingine vitengwe kwa ajili ya kuwekwa matawi ya taasisi za kibenki.

Amesema ili kurahisisha ufanyaji kazi na usalama wa fedha zao ni bora ofisi za kibenki ziwekwe kwenye soko hilo kama ilivyo soko la Geita ambapo wataweza kuendesha shughuri zao kiurahisi zaidi.



Aidha Miraji amesema ipo haja serikali kupitia wizara ya madini kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo juu yanuelewa wa matumizi ya kemikali migodini ili wajue matimizi sahihi kuhepuka mad hata.

Kwa upande wake Sayenda Haroun mnunuzi wa madini amesema licha ya kuhitaji taasisi za kibenki kuwepo kwenye soko hilo pia aliomba ofisi ya madini kuongeza kipimo cha madini kupunguza msongamano.



Haroun pia ameomba STAMICO kuwa karibu nao ili wanufaike na mashine za utafiti walizonazo ,hivyo serikali ilione jambo hili kwa jicho la ziada kuo ngeza tija ya uzalishaji.

Ombi lingine lililoombwa ni kuhusiana ushuru wa vifaa vya uchimbaji kama.Mitambo, Injini, Kemikali zipunguzwe ili wachimbaji wamudu gharama na wachimbe kisasa.

"Ndugu mwandishi hata mkulima ili aondokane na kilimo cha jembe la mkono ni lazime awezeshwe zana za kisasa, hata katika sekta ya madini hivyo hivyo" , amesema.



Afisa.madini mkazi mkoani Mbeya Laurent Mayala amesema maombi yaliyotolewa na wanunuzi hao wa dhahabu yana umuhimu hivyo yatapel ekwa kunako husika kuona namna ya kutatua.

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mbaraka Batenga ameyapokea maombi hayo na kudai kuwa kutokana na umuhimu wake atahakikisha yanafanyiwa kazi.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa