TCB BENKI YAUPIGA JEKI MKOA SONGWE VIFAA VYA MICJEZO




Na Ibrahim Yassin, Songwe

Katika kuendeleza tasnia ya michezo Mkoa wa Songwe, Benki ya Biashara Tanzania yaani Tanzania Commercial Bank (TCB), imetoa vifaa mbali mabli vya michezo kama jezi na mipira kwa mkoa wa Songwe.

Simon Mlelwa Meneja wa TCB Tawi la Mwanjelwa, Mkoa wa Mbeya, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Daniel Mihayo, alisema walipokea ombi la vifaa vya michezo katika kudumisha michezo.

“Na sisi kama TCB kila mwaka tuna utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii kutokana na kile tuna chekipata katika biashara tunayoifanya ya fedha, ili kuweza kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu,” amesea Mlelwa.



Amesema kuwa katika program ya kurudisha faida kwa jamii (CSR)imejikita katika maeneo matatu ambayo ni afya, elimu na ustawi wa jamii.

Kwa hiyo, kama maombi yaliowafikia benki hiyo wamefika leo kukabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni jezi pesa kadhaa na mipira katika kuhakik isha Mkoa wa Songwe mbele kimichezo.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amesema mkoa huo ni wa mwisho kuanzishwa nchini, kwa hiyo ni mkoa ambao ni less privileged region, huku akiipongeza TCB kwa msaada.



Kwa hiyo kuna mambo mengi ya msingi yanahitaji leadership kuyapushi ili yatokee, kwa vile ni moja ya mikoa michache ambayo haina timu ya ligi kuu.

“Sisi ndiyo viongozi wa kujenga misingi ili nasi siku moja tuwe na timu inayocheza ligi kuu Tanzalnia bara kutoka Mkoa wa Songwe…,” amesema Chongolo.

Wiki iliyopita RC Chongolo alikutana na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Songwe ili kueleza mikakati ya mkoa katika kunyayua michezo ili kuh akikisha michezo inakuwa ni sehemu ya maisha, hivyo kuwashukuru TCB kwa sapoti.


Naye, Meneja wa TCB Tawi la Tunduma Mkoa wa Songwe Julius Mlang’a amesema TCB kwa kutam bua umuhimu michezo wameguswa na kuweza kuchangia kile kidogo ambacho walipata kama faida na kurudisha kwa jamii, ili kuweza kuiguza jamii katika michezo.

“Michezo kwa sasa ni kipengele muhimu sana kwa sababu kupitia michezo inajemga utimamu wa akili, inaondoa stress, lakini pia michezo ni ajira na michezo ni afya,” ameelezea Mlang’a.



Amefafanua kuwa TCB imetoa seti za jezi na mipira yenye thamani ya Sh17.5 milioni ili kupitia michezo wanaenda kujenga maarifa mashuleni lakini pia katika kukuza vipaji na maadili mema kwa vijana pamoja na kujenga miili yao.

Kwa upande wake, Afisa Michezo Mkoa wa Songwe Mtaka Chibwi, ambaye pia ni katibu wa michezo katika kamati ya mkoa, ameipongeza TCB kwa vifaa vya michezo.

Ameelezea kuwa vifaa hivyo vitasadia katika kukuza na kuendeleza michezo katika Mkoa wa Songwe.


“Kama alivyosisitiza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo kwamba malengo yao ni kuwa na timu ya mkoa ambayo itaenda kucheza katika ligi kuu ya Tanzania bara.

Lakini pia vifaa hivi vitasaidia katika kukuza vipaji vya watoto wetu katika shule za msingi na sekondari,” amesema Chibwi.

Aidha, aliongeza kuwa kwa kuanzia wanaanza na ligi ya mkoa kuelekea kupata timu ya mkoa itaka yocheza ligi kuu kutokea Mkoa wa Songwe.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa