LEZENI ZA VITALU 1,505 ZA VIGOGO ZAFUTWA, MBELEMA KUNUFAIKA.



Na Ibrahim Yassin, Chunya

SERIKALI Kupitia wizara ya madini yafuta jumla ya leseni za vitalu 1505 wilayani Chunya mkoani Mbeya baada ya kutelekezwa na badala yake vitagawiwa kwa wachimbaji wadogo (MBELEMA).

Imeelezwa kuwa vitalu hivyo vilikua vikimilikiwa na wachimbaji wenye fedha nyingi (Madigala) na  utaratibu wa kuwagawia wachimbaji wadogo unafanyika.

Wilaya ya Chunya ni moja ya wilaya inayounda mkoa wa kimadini nchini ambayo asilimia kubwa ya uchumi wake unatokana na uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Hayo yamebainika  jana katika mahojiano na mwenyekiti mteule wa chama cha wachimbaji wadogo Saddam Kyando ofisini kwake wilayani humo.


Kyando amesema kitendo cha Serikali kutoa vitalu hivyo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyokuwa yakimilikiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha kimewafurahisha.

Ameeleza vitalu hivyo vitatoa fursa za kwa wachimbaji ambao wengi wao hawana leseni na kwamba kazi yao kwa sasa ni kuhamasisha wachimbaji kujiunga na Mbelema ili wasipitwe na fursa hiyo.

Amesema kupitia Leseni hizo uongozi umeanzisha matawi nanwatapita kila kata watatumia ofisi za watengaji kata kuhamasisha wachimbaji kujiunga na chama.


"Kipindi hiki hatutaki kuandamana na ndiyo maana tunataka kuwakutanisha wachimbaji kuwa.kitu kimoja ili changamoto zao na mambo yote yamaliziwe ofisini " amesema Kyando.

Hata hivyo Kyando katika uongozi wake ameahidi kujenga ofisi kuu ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kununua usafiri ili kurahisisha shughuli zao na hata yanapotokea majanga maeneo ya kazi waweze kuwafikia kwa haraka.

Nae mjumbe wa umoja wa wanunuzi wa dhhabu Chunya Msabira Miraji amesema pamoja na mikakati mizuri ya serikari kuboresha sekta hiyo aliomba kwenye soko la madini zifunguliwe huduma za kibenk kurahisisha utendaji na usalama wa fedha zao.

Afisa madini Mkazi mkoani Mbeya Laurent Mayala amesema serikali imefanya jambo kubwa kwa kuwajali wachimbaji ambao wengi wao hawakuwa na maeneo ya kuchimba.

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mbaraka Batenga amesema Leseni za vitalu hivyo zimenyang"anywa kwa kuwa maeneo hayo yalikuwa hayatumiki huku wachimbaji wadogo wakikosa maeneo.

Amesema wilaya ya Chunya imebarikiwa kuwa ni mikoa miwili yaani mkoa wa kimadini na mkoa wa Kitumbaku lakini bado hakuna wachimbaji wakubwa waliopo ni wadogo ila wanatofautiana mitaji.


Amesema mikakati iliyopo ni kuhakikisha wachimbaji wadogo wanajengewa uwezo ili wafanikishe malengo yao na serikali ipate kipato kwani asilimia zaidi ya 30 ya pato la Taifa linatoka kwenye madini.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa