Huduma bora za afya zapunguza vifo vya Mama na Mtoto
Hospitali ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kwa kipindi cha miezi sita imewezesha wanawake 860 kujifungua kati yao wanawake 741wakijifungua kwa njia ya kawaida na 119 wakijifungua kwa njia ya upasuaji huku vifo vya mama na mtoto vikipungua kutoka 11-8 kwa mwaka 2023.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa huduma za mama na mtoto wilayani humo Bakari Ndarusi wakati wa utoaji elimu kwa wanawake wanao jifungua katika hosptali hiyo,ambapo amesema licha ya hilo hospitali hiyo inahudumia wastani wa watoto 180 hadi 200 na watoto njiti 6 kwa kila mwezi.
Aidha amesema hospitali hiyo inahudumia wanawake wanaojifungua wapatao 8-9 kwa siku na kubainisha kuwa hadi kufikia march 2024 wanawake 2218 wamepatiwa huduma za Mama na mtoto na kwamba kila mwezi Wanawake 164 wamekuwa wakihudhuria huduma hizo .
Kwa upande muuguzi mkuu wa hospitali hiyo , Diana Didi amesema licha ya hilo hospitali hiyo imekuwa ikihudumia wanawake 30 kwa siku na kuwataka wanawake kujenga mazoea ya kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapopatwa na uchungu wa kujifungua ili kuokoa vifo vya mama na mtoto.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sunday Wambula akiwa ofisni kwake amebainisha kuwa licha ya hilo halmshauri imepokea fedha millioni mia nne kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati 8 na shilingi million mia tatu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vituo vipya vya afya.

Comments
Post a Comment