JINSI VIJANA WALIVYOENDELEZA MAISHA YAO KUPITIA KAMPUNI YA LIMA KWANZA WAKIWAASA MACHANGUDOA.

                  MAKALA

WANAWAKE WANAOJIUZA WAPEWA MCHINGO KUINUA VIPATO VYAO.



Na Ibrahim Yassin,Songwe

Imeelezwa kuwa vijana wakiwemo wanawake nchini wametakiwa kutojiingiza kwenye kazi za hatari zikiwemo za wizi,Uharifu na ukahaba na badala yake wametakiwa kujiingiza kufanya kazi za viwandani ili wajipatie kipato hahali.

Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa iliyojaliwa kuwa na Viwanda vingi vikiwemo vya uchakataji wa mazao ambapo kiwanda kilichopo kwenye kampuni ya Lima Kwanza pekee kikiajiri vijana zaidi ya 300 wanaofanya kazi mbalimbali na kujiingizia kipato.

Uwepo wa viwanda ni moja sababu ya kupunguza uzururaji na ukahaba ikiwemo uharifu,kwani vijana wengi wakiingizwa kufanya kazi viwandani matukio ya kiharifu yatapungua na hata kutokomezwa kabisa.

Kumekuwa na kawaida kwa akina dada wengi hasa wenye umri mdogo kujiingiza kwenye kufanya kazi Baa na wengine wakiingia kwenye mkumbo wa kuuza miili yao kwa wanaume kwa ajili ya kupata fedha zinazotajwa ni haramu.

Kwa upande wa vijana wengi wao wamekuwa wakijiingiza kwenye kazi zisizofaa ikiwemo wizi na ubakaji na kujikuta wanaishia jela ni kutokana na kutokuwa na kazi inayowaingizia kipato,ambao wameshauriwa wakaombe kazi kwenye kampuni zilizopo maeneo yao ili waweze kubadirisha maisha.

Kampuni ya Lima Kwanza Limited iliyopo kijiji ma kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani hapa ni moja ya kampuni ya kizalendo iliyojishughurisha na uchakataji wa mazao ya Kahawa,Parachichi,Makidonia na mazao mengine.

Mbali na mazao hayo,pia wananunua mazao hayo ikiwemo parachichi ambayo hukamuliwa na mafuta yake usafirishwa kwenda nje ya nchi hali iliyowanufaisha wakulima wa vijiji hivyo ambao awali mazao yakiiva yanaoza na baada ya ujio wa kiwanda hicho wamekuwa wakivuna na kuuza.

Uwepo wa viwanda mkoani Songwe umeweza kupunguza lindi la vijana wakiwemo wanawake kubweteka kwani wengi wao wamekuwa wakipata ajira za mikataba na fedha wanazozipata wamekuwa wakiendesha maisha yao ya kila siku.

Shungu Yusuph mkazi wa Vwawa anasema aliajiriwa kwenye kampuni hiyo miaka 3 iliyopita ameweza kumudu ghara ya chuo cha maendeleo ya jamii kwe kumlipia fedha mwanae na michango mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Sumeda Alcado mkazi wa Mbozi,anasema yeye ana miaka mmoja na nusu toka apate ajira kwenye kiwanda hicho,kutokana na mshahara anaoupata ameweza kumuda gharama ya kumsomesha mtoto wake kidato cha tano.

Mfanyakazi mungine ni Medo Mwazembe aliyefikisha miaka miwili kufanya kazi kwenye kiwanda hicho,anasema kwa mshahara anaoupata ameweza kusomesha watoto wawili na amenunua mifuko kadhaa ya saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya wazazi wake.

Happy Nzunda mkazi wa Vwawa anasema amedumu kwenye kiwanda hicho kwa muda wa miaka 5,mshahara anaoupata anamudu kuwalea wazazi wake kwa kuwapa mahitaji mbalimbali,anasomesha,na sasa amefyatua tofari na kuanza ujenzi wa nyumba ya kuishi.

''Akina dada wengi wamekata tamaa ya ,maisha wamekuwa wakijiingiza kwenye kazi za ukahaba na kuhatarisha afya na maisha yao,ni bora wangeenda kuomba kazi kwenye kampini zilizopo maeneo yao ili waweze kumudu kuendesha maisha yao na si hivi wanavyouza miili yao na kuwa na maisha ya hofu, waje waombe kazi ''anasema Nzunda.

Nae John Kibona mkazi wa Masangula,anasema anamiaka 2 na nusu toka apate ajira kwenye kampuni ya Lima Kwanza,kuputia mshahara anaopokea ameweza kujenga nyumba,kununua na kufuga kuku na Nguruwe,kununua miche 1000 ya kahawa na kuwalipa vibarua wanaompandia shambani kwake.

Anasema kutokana na manufaa wanayoyapata kwenye kiwanda hicho kilichopo ndani ya kampuni ya Lima Kwanza Limited,wameondokana na kujiingiza kwenye uharifu na hata wanawake kujiingiza kwenye ukahaba,hivto anawaomba vijana wenzake wakaombe kazi ili wainue vipato vyao.

Akizungumzia hali hiyo,Meneja wa kampuni hiyo,Vicent Samwel,anasema kazi kiwanda cha lima kinajishughurisha na uchakataji mazao na hata kulima,kwani wanamashamba yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 150.

Anaema vijana wengi hasa akina mama wanafanya kazi ya kuchambua kahawa iliyokaushwa hyuku wengine wakifanya kazi mashambani ambao wanawalipa kwa wakati hali inayopelekea waweze kumudu maisha yao na familia zao.

Kwa upande wa ushiriki kwenye jamii,Samwel anasema wameweza kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo afya,elimu na miundombinu ya barabara na kwamba hivi juzi tu walitoa madawati 450 shule ya msingi masangula,pamoja na mifuko ya saluji kwenye na mipira shule ya msingi Ilengo zinazozunguka kiwanda.

‘’Tumekuwa tukishiriki kazi za kijamii mara kwa mara,na hata kukarabati barabara kwenye sehemu korofi na zinapitika vizuri muda wote, bado tunapokea vijana wanaohitaji kufanya kazi kiwandani hapo hasa wakati wa kiangazi kipindi cha kuvuna’’Anasema Samwel.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Lima Kwanza Limited, Tinson Nzunda,anasema kiwanda chake kimekuwa kikitoa ajira kwa vijana wa kada mbalimbali kwa ajili ya kazi mbalimbali zilizopo ikiwemo kuvuna Kahawa,Maparachichi,Makademia na kuyakausha juani hadi kutunza gharani.

Anasema Parachichi huwa wanakamua mafuta yake wanayauza kwenye nchi za Ulaya,zao hili limekuwa na faida hasa kwa wakulima ambao walikuwa wakiyatupa pindi yanapoivu lakini ujio wa kiwanda hiki wamekuwa wakiyaleta na kuyauza na kujipatia kipato.

Kwa upande wa zao la Kahawa wao wakichakata wanauza kwenye soko la pamoja Tanzania (TCB) na zao la Makadenia (Karanga Pori) wanauza kwenye masoko ya ndani na wao licha ya kulima pia wananunua kwa wakulima wengine.

Anaongeza kuwa licha ya kampuni hiyo kuajiri vijana zaidi ya 300 pia wamekuwa ni walipaji wazuri wa kodi na kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii kwenye vijiji vinavyozunguka kiwanda na hata asilimia kubwa ya walioajiriwa ni vijana wanaozunguka Kiwanda.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa