WANAWAKE WATAKIWA KUTOJIINGIZA KWENYE KAZI ZA KUJIUZA,WAOMBE KAZI VIWANDANI.

Na Ibrahim Yassin,Songwe

WANAWAKE wa wilaya mbalimbali zilizopo mkoani Songwe,wametakiwa kuacha tabia ya kujiuza miili yao kwa wanaume kama ni njia ya kujipatia kipato na badala yake waombe kazi kwenye kampuni mbalimbali zitakazowatoa kwenye lindi la umasikini.

Kauli hiyo imetolewa  Machi 14/2024 na  Vicent Samwel,Meneja wa kampuni ya Lima Kwa nza Limited inayojishughulisha na uchakataji na usindikaji mazao ya kahawa na Parachichi kwe nye kijiji na kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani humo.

Samwel amesema mkoa wa Songwe unajiwanda vingi ambapo vijana wengi wakiwemo wana wake wanafanya kazi za mikataba na kujiinua kiuchumi hivyo wanawake wanaotegemea kuuza miili yao (Kudanga) ili wapate fedha waache na waombe kazi viwandani.

Alisema kampuni ya Lima Kwanza inayoongozwa na Mkurugenzi mtendaji Tinson Nzunda imetoa ajira kwa vijana na wanawake zaidi ya 300 wanaofanya kazi ya kuchambua kahawa na parachichi huku wengine wakiwa mashambani wamevuka hatua kubwa kutokana na mishahara waipatayo.



Aliongeza kuwa kampuni bado inahitaji vijana hasa wanawake,hivyo vijana wanaokaa vijiweni na kupiga soga na wanawake wanaofanya kazi ya kujiuza miili yao wanatakiwa waachane na kazi hiyo na badala yake waombe kazi za mikataba kwenye kampuni zilizopo.

‘’Kampuni ya Lima Kwanza licha ya kujihusisha na kilimo cha mazoa ya Parachichi na Kahawa pia inanunua mazao hao kwani awali parachichi zilikuwa zikioza wananchi hawakujua pahala pa kuuza,ujio wa kiwanda hicho umekuwa ni mkombozi kwao baada ya wao kuvuna na kuwauzia’’amesema.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya Lima,Tinson Nzunda amesema ajira nyingi walizotoa ni vijana wanaozunguka kiwanda hicho licha ya kuwa wapo wanaotoka Mbozi na Mlowo na kwamba wamewaingiza kwenye mabenki na wanakopesheka.

Shungu Yusuph (40) mkazi wa Vwawa,amesema alipata ajira kwenye kiwanda hicho miaka 3 iliyopita kutokana na mshahara anaoupata anasomesha mtoto chuo cha maendeleo ya jamii,na amefanikiwa kujenga nyumba na kufanya ufugaji wa nguruwe na kuku.



Naye Medo Mwazembe (26) Mkazi wa Mbozi,amesema ameajiriwa kwenye kampuni hiyo miaka 4 iliyopita ameweza kujenga nyumba,kusomesha watoto 2,na kununua shamba na kupanda Kahawa,anawashauri vijana wenzake wasikae vijiweni na hata akina dada wanaodanga waombe kazi viwandani


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa