TAG kuadhimisha miaka 85 toka kuanzishwa kwake kwa mafanikio makubwa
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
KANISA la Assemblies Of God Tanzania (TAG) wilaya Nkasi mkoani Rukwa linatarajia kufanya matendo mbalimbali ya kijamii na ya huruma katika kuelekea maadhimisho ya miaka 85 toka kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa Nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana Makamo mwenyekiti mwangalizi wa kanisa hilo sehemu ya Nkasi na mchunbgaji wa kanisa hilo Nkomolo Efraimu Lyandulu amesema kuwa wao kama kanisa katika kuelekea maadhimisho ya miaka 85 ya kanisa hilo watashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya matendo mbalimbali ya huruma.
Amesema kuwa kwanza wanatarajia kutoa mifuko 10 ya saruji kwa shule ya msingi Nkomolo kama sehemu ya mchango wao kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni pamoja na kwenda kuwatizama Wafungwa katika gereza la Kitete liliopo wilayani Nkasi.
Alidai kuwa kanisa kama taasisi ukiachana na mambo ya kiroho ambayo yamekuwa yakifanyika kwa asilimia kubwa lakini pia linalo jukumu la kuhakikisha maisha ya jamii yanakua bora kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana ikiwa ni pamoja na jamii kuhakikisha kuwa wanafanya kazi na kuweza kujiletea maendeleo.
Mchungaji Lyandulu amefafanua kuwa kanisa hilo limeanza rasmi hapa nchini toka mwaka 1939 na lilianzia Igale jijini Mbeya chini ya Mmisionari wa kwanza wa kujitegemea kutokea Marekani Paul Derry na kanisa hilo likaendelea kukua Nchi nzima na kuendelea kuhubiri injili na kukemea maovu katika jamii.
Amesema kuwa kanisa la TAG katika miaka 85 limefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuhubiri na kukemea mabaya ambayo yamekua yakijitokeza katika jamii kama vile Ulevi,uwizi,Uvivu,ushirikina na mtendo mengine mabaya yanayofanana na hayo katika kuleta utengamano katika taifa ikiwa ni pamoja na kuziponya roho za Watu ili mwisho wa siku waweze kuurithi ufalme wa Mungu.
Pia amedai kuwa kanisa hilo limeendelea kukua katika maeneo mbalimbali ya wilaya Nkasi na kuwa ambapo kwa sasa limeenea katika maeneo mbalimbali na mpaka sasa wana maeneo Manne ya kanisa hilo ambalo ni Namanyere Magharibi,Eneo la Kasikazini,Eneo la kusini ikiwa ni pamoja na eneo la Chala.
Kanisa hilo la TAG toka kuanzishwa kwake hadi sasa limeongozwa na viongozi wakuu wa kitaifa Watatu ambao ni Askofu Emmanuel Razaro,Ranuel Mwanisongole na Dkt,Barnabasi Mtokambali ambaye ndiye anayeliongoza kanisa hilo hadi sasa.


Comments
Post a Comment