MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WATAJA CHANGAMOTO ZA FAINI WAKIPIGWA MSASA NA LATRA


Na Ibrahim Yassin,Songwe

Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuheshimu sheria za barabarani kwa kutozidisha abiria ikiwemo utoaji wa tiketi kwa abiria ili kuepuka kulipishwa faini zisizokuwa na tija na kuhatarisha usalama wa abiria.

Imekuwa ni kawaida kwa madereva na makondakta hasa nyakati za sikukuu kuvunja sheria kwa tamaa ya kupata fedha nyingi kwa kujaza abiria kupita kiasi licha ya kuwa sharia inawataka wapakie kulingana na idadi ya viti.

Kauli hiyo imetolewa leo Disemba 19/ 2025 na mkaguzi wa polisi ofisi ya mkuu wa usalama barabarani wilayani Mbozi mkoani Songwe Anthony Sabasaba katika mafunzo siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa jeshi la polisi mkoani Songwe chini ya maafisa sharia kutola Latra makao makuu.

Amsema wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara na kukuta makosa yanayojirudia ikiwemo makondakta kuto toa tiketi,kujaza abiria kupita kiasi na baadhi ya madereva wakibainika Leseni zao kuisha muda wake.

Amesema maafisa wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri aridhini (LATRA) wametoa elimu ya kutosha hivyo anaamini madereva na makondakta watafuata sharia za usalama barabarani na hali itakayopunguza ajari zisizokuwa za lazima hasa kipindi hiki cha sikukuu.



Akizungumza kwa niaba ya madereva katika kikao hicho,Sai Danki,amesema mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini inatumia vigezo vipi kutoza faini za Laki 5 hadi Milioni 1 pindi wanapokuta makosa kwenye magari akidai faini hizo ni kubwa kuliko kipato wanachokikusanya.

Martha Ngaga afisa sharia wa Latra kutoka makao makuu jijini Dodoma katika mafunzo hayo aliwataka wamiliki wa vyombo vya moto kuwa kitu kimoja na madereva na makondakta katika kuzingatia sharia za barabarani.

Amesema wao ni wadau muhimu na ndiyo maana wamekuwa wakiwashirikisha katika kila hatua hasa ya sharia ya mabadiliko ili kuenda sambamba na takwa la serikali la kuhakikisha wanaondoa ajari za barabarani.

Kauli hizo zimekuja baada ya Dereva Sai Danki kuhoji sababu ya mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini kuwa inatumia vigezo vipi kutoza faini za Laki 5 hadi Milioni 1 pindi wanapokuta makosa kwenye magari akidai faini hizo ni kubwa kuliko kipato wanachokikusanya.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa