SONGWE YA DKT.SAMIA YAJIVUNIA KUPAA SEKTA YA ELIMU,AFYA NA MAJI WATAKA MAFANIKIO ZAIDI AWAMU HII

                                  MAKALA
Na Ibrahim Yassin,Songwe

RIPOTI MAALUM.
WAKATI wananchi wa wilaya nne zilizopo mkoani Songwe wakijivunia mafanikio ya awamu ya 6 iliyopita katika sekta ya Elimu,Afya na Maji,wananchi hao wamejenga Imani ya kupata mafanikio zaidi katika awamu hii.

Mkoa wa Songwe ulioanzishwa mwaka 2016 ukimegwa kutoka mkoa wa Mbeya na jina la mkoa limetokana na mto Songwe huku makao makuu yake yakiwa Vwawa wilayani Mbozi.

Mkoa huu ukiwa nae neo lake la Kilometa 27,656 linapakana na nchi za Zambia na Malawi kwa upande wa kusini,Mji wa Tunduma ndiyo lango kuu la kuingilia nchini Zambia na Isongole Ileje ndiyo lango kuu la kuingilia nchini Malawi.

Mikoa jirani na mkoa wa Songwe ni Rukwa na Katavi upande wa Magharibi,Tabora upande wa Kaskazini, na Mbeya upande wa Mashariki,Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi waliohesabiwa ni 1,035,214,na asilimia 80 ya wananchi wa mkoa huu hutegemea kilimo na ufugaji.

MAFANIKIO SEKTA YA ELIMU.

Wakati Rais Dkt,Samia anaingia madarakani alikuta wanafunzi wanaosoma shule za awali na msingi wapo 270,784 ambapo kwa sasa baada ya kuongeza miundombinu idadi ya wanafunzi wanaosoma shule za awali na msingi imeongezeka na kuwa 286,189.



Pia alikuta idadi ya walimu wa naofundisha shule za awali na msingi wakiwa 3,874 lakini baada ya maboresho ya miundombinu idadi hiyo ya walimu iliongezeka na kuwa 4,074.

Taarifa zinaonesha kuwa kabla ya mwaka 2021 mkoa ulikuwa na shule za shule za sekondari 120 lakini utawala wa awamu ya sita ulifanikisha kuongeza shule na kuwa 153.

Na pia idadi ya wanafunzi wanaosoma shule za sekondari kabla ya utawala wa awamu wa sita kuingia madarakani mwaka 2021 ilikuwa 52,097 lakini baada ya maboresho ya miundombinu idadi imeongezeka na kuwa wanafunzi zaidi ya 57,242 wanaosoma bila malipo.



Aida Rais Dkt,Samia alipokuwa akiingia madarakani alikuta wanafunzi wa shule za sekondari wanafundishwa na walimu 1,836,lakini baada ya maboresho ya miundombinu idadi ya walimu imeongezeka na kuwa 3,873.

Akiwa katika mwaka wa pili wa utawala wake wa awamu ya sita Rais Dkt,Samia alitumia Tilioni 1.29 kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule zote nchi nzima.

Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 454.3 zilitolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za elimu ya awali na msingi.



Utolewaji wa fedha hizo zilitumika kujenga shule mpya Bilioni 342,Vyumba vya madarasa 9,189,Nyumba za walimu 346, Mabweni 28 na ukarabati wa shule kongwe 45 nchi nzima.

Dkt,Samia pia katika awamu hiyo ya sita alianzisha ujenzi wa shule mpya 184 za sekondari za kata ambapo kila halmashauri nchi nzima alijenga shule moja.

Aidha Dkt,Samia alitoa wastani wa Milioni 600 kwa kila halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa shule hizo,ujenzi ulioambatana na nyumba za walimu na kununua vifaa vifaa vya Tehama vya kujifunzia nchi nzima.



Mbali na ujenzi wa shule hizo 184 kila kata nchi nzima,Rais Dkt,Samia pia alianzisha ujenzi wa shule za wasichana za sayansi,ambapo shule moja kwa kila mkoa nchi nzima ambapo alieleza kuwa zikikamilika ataanza kujenga shule za wavulana.

SEKTA YA MAJI MKOA .

Katika utawala wa awamu ya sita miradi ya maji iliongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 79.9 mwaka 2024.

Katika kutimiza azma hiyo,Dkt,Samia ametekeleza na kukamilisha jumla ya miradi 164 kati ya miradi 177 ambayo haikukamilika katika awamu zilizopita licha ya serikali kutoa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika miradi ya kimkakati Dkt,Samia pia ametekeleza miradi 28 ya maji na miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.



Ili kukabiliana na kero ya maji kwa wananchi Rais Dkt,Samia alianzisha ujenzi wa kuchimbavisima 900 vya maji saw ana visima vitano kwa kila jimbo ambavyo vingine vimekamilika na vingine vipo hatua za mwisho,

Aidha uongozi wa Rais Dkt,Samia pia umeanzisha huduma ya kufunga mita za maji za lipa kabla ya mtumizi { Pre Paid ) kwenye taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Hatua hiyo inakusudia kumaliza malalamiko ya wanachi kuhusu kubambikiziwa Ankala za maji na kuhakikisha Taasisi hizo zikiwemo zikiwemo za Majeshi zinalipia gharama za maji kulingana na matumizi yake.

Katika hali ya kumtua mama ndoo kichani Rais Dkt,Samia wakati anaingia madarakani alikuta hali ya upatikanaji wa maji ukiwa asilimia 54.3 vijijini na asilimia 44.5 mijini lakini leo upatikanaji wa maji safi na salama vijijini ni asilimia 78.8 na  asilimia 70.6 mijini.

SEKTA YA AFYA .

Rais Dkt,Samia wakati anaingia madarakani mwaka 2021 katika awamu ya sita alikuta vituo vya kutolea tiba vipo 205 lakini hivi sasa vipo 263 katika mkoa mzima.

Kati ya vituo hivyo, hospitali zipo 10 sawa na asilimia 3.8,vituo vya afya vipo 23 sawa na asilimia 8.7 na zahanati 230 sawa na asilimia 87.5.



Miungoni mwa vituo hivyo vya kutolea tiba, vituo 214 ni vya serikali saw ana asilimia 81.4 na vituo vya binafsi vikiwemo vya Taasisi za dini vipo 49 sawa na asilimia 18.6.

Rais Dkt,Samia pia amewekeza kwenye afya msingi katika Zahanati na vituo vya afya ambapo Zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanatibiwa.

Mbali na Rais Dkt,Samia kujenga vituo hivyo,pia amepeleka magari mawili mapya ya wagonjwa kila halmashauri mkoa mzima wa Songwe zikiwemo Toyota Land Cruiser Hardtop moja kwa kwa huduma za afya mkoa nchi nzima.

Maboresho hayo katika sekta ya afya yamepunguza vifo vya mama wajawazito kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai 100.000.



Aidha vifo vya Watoto wenye umri chini ya miaka 5 navyo vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000.

Ikiwa mafanikio makubwa yaliyopatikana awamu ya sita katika sekta hizo,wanannchi wanamatumaini makubwa ya kuona mafanikio makubwa Zaidi katika kipindi hiki kingine cha utawala wa Rais Dkt,Samia akisaidiwa na makamu wake Dkt,Immanuel Nchimbi na waziri mkuu Dkt, Mwigulu Nchemba.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa