MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO NA WAMILIKI WAPEWA SOMO UTII WA SHERIA NA KANUNI KWENYE VYOMBO VYA MOTO
- Get link
- X
- Other Apps
Na Ibrahim Yassin,Songwe
IMEELEZWA kuwa vitendo vya kupandisha bei za nauli na kujaza abiria kupita kiasi katika magari yanayosafiri umbali mrefu umetajwa kuhatarisha usalama wa abiria uneopelekea uwepo wa ajali za mara kwa mara imebainika.
Imekuwa ni kawaida kwa madereva wa vyombo vya moto siku za sikukuu wakizitumia kama fursa za kujipatia kipato kikubwa kwa kuvunja sheria kwa kupandisha nauli na kujaza abiria kupita kiasi bila kujari kuwa wanaweza kusababisha maafa.
Miaka yote inapofika mwisho mwa mwaka katika sikukuu za Chrismas na mwaka mpya tumeshuhudia uwepo wa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na uzembe na tamaa ya madereva na makondakta.
Maeneo mengi ya stendi za mabasi yaendayo mikoani hujumazimekuwa zikifanyika baada ya wakatisha tiketi kupandisha nauli baada ya uwepo wa abiria wengi wanaoenga mapumzikoni na hata shule zinapo funga.
Mbali na hilo pia kumekuwa na uzembe wa wazi wazi unaofanywa na baadhi ya makondakta kwa kutowapa tiketi abiria huku baadhi ya madereva wakifanya kazi kwa mazoea kwa kutolipia Leseni pindi zinapoisha muda wake.
Kwa upande wa wamiliki wa vyombo vya moto pia wamekuwa wakikosa elimu na matumizi sahihi ya ving’amuzi huku wakiendelea kuwalalamikia madereva wa magari yao pindi wanapoona gari linatozwa faini za mara kwa mara.
Kutokana na uwepo wa makosa hayo, Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Kupitia kwa maafisawake wa kitengo cha sheia makao makuu wameanza kuoa semina elekezi kwa madereva wa vyombo vya mto na wamiliki ili kuondoa changamoto za ajali barabarani.
Maafisa hao,jana walikuwepo mkoani Songwe wakitokea mkoani Rukwa ambapo waliendesha semina elekezi kwa maafisa usafirishaji,madereva wa nyombo vya moto na wamiliki,mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa jehsi la polisi mkoani Songwe.
Mafunzo hayo yalishirikisha jeshi la polisi usalama barabarani,Jeshi la zima moto,maafisa wa Latra mkoa na Taifa dhidi ya madereva na amiliki wa vyombo vyote vya moto yaani Magari,Pikipiki,na bajaji pamoja na maafisa usafirishaji.
Akifungua kikao hicho Meneja wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) mkoani Songwe,Joseph Bulongo alisema lengo la mafunzo hayo ni kukumbushana na kupeana kanuni 6 za sheria za uendeshaji vyombo vya moto.
Baada ya kufungua kikao hicho,Afisa sheria wa Latra kutoka makao makuu Matha Ngaga alisema baada ya kuona sheria nyingi zinakiukwa wameamua kupita kila mkoa nchini kukumbushana na kuelezea uwepo wa kanuni sita.
Alisema kanuni hizi zitajulikana kama kanuni za uwezeshaji wa watoa huduma za usafirishaji za mamlaka udhibiti usafiri ardhini za mwaka 2024.
Aliongeza kuwa kanuni hizi zitatumika pia kwa wawezeshaji wa huduma za za usafirishaji wa abiria na mizigo kupitia mfumo,usimamizi au kwa namna yeyote ya uwezeshaji.
Alisema mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini iliyoanzishwa chini ya sheria ya mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini,maana yake ni mtu au kampuni inayojitegemea ambayo inayotoa huduma kwaniaba ya mtoa huduma.
Pia aliwaeleza wajumbe hayo kuwa mtu atakayekusudia kutoa huduma ya uwezeshaji atapaswa kuomba kusajiliwa kwa mamlaka kwa kujaza fomu iliyoainishwa na mamlaka.
Alisema mtoa huduma atakaye sajiliwa katika kanuni hizi wezeshi ataweza kusaidia ukataji wa tiketi mtandaoni,kusaidia kufanya maombi katika mfumo wa leseni za mamlaka,ufungaji wa vifaa vya ufuatiliaji mwendo wa chombo,uwakala wa mabasi na ukusanyaji na usambazaji mizigo.
Baada ya kueleza hivyo wajumbe walianza kuhoji mapungufu yaliyopo,ambapo mwenyekiti wa waendesha bodaboda mkoani Songwe,Omary Mbuba,alisema anapongeza kwa elimu hiyo,pia aliomba ufafanuzi juu ya mawakala wa kukatisha Leseni kufanya msako mitaani.
Mbuba alisema imekuwa ni kawaida kwa mbia aliyepewa uwakala kuendesha msako mitaani na kukamata pikipiki au bajaji zisizokuwa na Leseni hali inayozua taharuki na kusababisha ajali kuhu mawakala hao wakivalia nguo zenye nembo za Latra.
Nae Elia Kibona mmiliki wa magari licha ya kupongeza uendeshaji wa mafunzo hayo aliwataka maafisa hao kupunguza gharama za faini huku akiwataka wamiliki wenzake kuona umuhimu wa kufunga ving’amuzi kwenye magari yao.
Naye Sai Padwi dereva alisema mamlaka inatumia vigezo gani kuwatoza faini kati ya laki 5 hadi milioni 1 pindi wanapowakuta na makosa barabarani,huku akihoji kuwa faini hizo ni kubwa kuliko makusanyo wanayoyapata.
Elly Songuo Kaim katibu wa wamiliki wa kosta mkoa,alisema sheria nyingi zinazotungwa na Latra io shirikishi kwao,na pia mazingira ya barabara nyingi ni mbovu hivyo wanapata ukakasi wanapoambiwa watumie teckolojia zaidi.
Kwa upande wake mmiliki wa magari ya Maribwa mkoani humo,Thobias Maribwa alisema magari ya kutoka tunduma kwenda Mbeya abiria wengi wanapandia njiani,lakini wamekuwa wakitozwa faini kwa madai kuwa hawajakata tiketi huku akiomba ufafanuzi wa jambo hilo.
Akizungumzia suala la faini kwa dereva anayeendesha mwendo mkubwa Anthon Sabasaba mkaguzi wa usalama barabarani kutoka ofisi ya wilaya ya Mbozi,alisema wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara na kugundua makosa yanayojirudia rudia.
Alisema kwa dereva atakayeendesha mwendo kuanzia spidi 86 hadi 99 kisheria anatozwa faini na atakayeendesha spidi 100 na kuendelea adhabu yake ni kunyang’anywa Leseni na kwamba faini hizo zimewekwa ili madereva waongeze umakini barabarani.
Nae meneja wa Latra mkoani Songwe Joseph Bulongo alisema lalamiko lililotolewa la ulipishwaji wa faini kuanzia laki 5 hadi Milioni 1 kuwa haijawahi kulipishwa na kuwa faini zinazolipishwa ni za kawaida na huwa mmiliki wa chombo anapatiwa taarifa la kosa lenyewe.
Alisema pia ni muhimu kwa mmiliki wa chombo kufunga king’amuzi kwani atatambua gari lake lilipo au limesafiri mara ngapi akiwa nyumbani, nahata dereva anapotozwa faini mmiliki atatambua kosa lililotokea akiwa nyumbani.
Aliongeza kuwa kwa mmiliki anayetaka kufunga king’amuzi na kupewa leseni anatakiwa kufika ofisini kupewa utaratibu atajaza fomu na kuelezwa namna ya kulifuatilia gari lake popote litakapokuwa.
Irene Sawe afisa sheria mkoa kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) alisema ni muhimu madereva na makondakta kufuata sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhepuka kutozwa faini kila wakati.
Martha Ngaga afisa sheria kutoka Latra makao makuu yaliyopo jijini Dodoma pamoja na mambo mengine alisema ni kosa kwa mtu ama kikundi kilichopewa uwakala wa kukatisha Leseni za vyombo vya moto kusanya msako wa kukamata chombo chochote.
Alisema wakala aliyepewa tenda anatakiwa akae ofisini kwake kukatisha Leseni na si kuzunguka mitaani kukamata pikipiki au bajaji na kutoza faini huku wakivalia ngua zenye nembo za Latra akidai hilo ni kosa kisheria.
Pia aliwataka madereva kuwa makini na kuacha kuwapatia magari yao yaendeshwe na madereva vishoka wasio kuwa na Leseni siku za juma mosi na juma pili hali hiyo inaweza sababisha ajali na uvunjifu wa kanuni zilizowekwa.



Comments
Post a Comment