Wazee wamtwisha zigo la migogoro ya ardhi diwani wa Nkomolo



Na Israel Mwaisaka,Nkasi
‎Wazee wa kata ya Nkomolo wilayani Nkasi wamemtaka diwani wa kata hiyo Sitivine Tontololo kuahakikisha analiangazia tatizo la migogoro ya ardhi ambalo limeendelea kuwa tatizo kubwa katika eneo Hilo.
‎Wamesema kuwa licha ya serikali na wadau wengine kufanya jitihada mbalimbali za kuondoa tatizo Hilo lakini bado tatizo la migogoro ya ardhi halijatafutiwa ufumbuzi.


‎Hayo yamezungumzwa leo na Wazee baada ya diwani huyo kuwakutanisha Wazee wa kata ya Nkomolo na kutaka wamueleze changamoto zilizopo kata ya Nkomolo ikiwa ni pamoja na kutizama vipaumbele atakavyoanza navyo kama diwani baada ya kuchaguliwa hivi karibuni
‎Mwenyekiti wa Wazee wa (CCM) wilaya Nkasi Permin Matumizi amemuomba diwani huyo kuanza na jambo hilo la migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kufuatilia fidia serikalini kwa watu ambao mazao Yao yameharibiwa na Wanyama waharibifu wakiwemo Tembo baada ya kata hiyo kupakana na hifadhi

‎Diwani Tontololo amewashukuru Wazee hao kwa kumueleza changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kumpa baraka za kuanza na kazi hiyo ya uwakilishi wa Wananchi katika kata ya Nkomolo

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa