MADEREVA NA WAMILIKI WA PIKIPIKI NA BAJAJI WAHOJI SABABU YA WALIPISHA LESENI KUKAMATA NA KUTOZA FAINI VYOMBO VYAO.



Na Ibrahim Yassin,Songwe

MARUFUKU yatangazwa kwa wanaochukua tenda za kulipisha Leseni za bajaji na pikipiki kufanya msako wa kuwakamata wasiolipa Leseni na kuwatoza fedha zinazodaiwa kuwa ni Rushwa ikidaiwa hakuna sharia inayowaruhusu kufanya hivyo.

Marufuku hiyo imetolewa hivi karibuni katika semina elekezi iliyotolewa na maafisa wa sharia wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA) katika ukumbi wa jeshi la polisi uliopo mkoani Songwe ukihudhuriwa na wamiliki wa vyombo vya moto, madereva.makondakta na jeshi la polisi usalama barabarani.

Katika kikao hicho mwenyekiti wa waendesha bodaboda mkoani Songwe Omary Mbuba ,amesema wanapongeza elimu iliyotolewa ya usalama barabarani lakini wanataka kujua sababu ya waliopewa tenda za kukamata pikipiki zisizo na Leseni na kusababisha ajali.

Amesema waliopewa tenda za uwakala wa kukatisha Leseni wamekuwa wakivaa sale zenye nembo za LATRA na kukimbizana na waendesha pikipiki na bajali kufanya ukaguzi na kusababisha ajali hali ya kuwa sharia haiwaruhusu na hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao.

‘’Ndugu muwezeshaji,kila kijiwe cha boda boda kina viongozi wake,kama mmewapa mamlaka hayo ni bora ngetueleza ili kukwepa migongano iliyopo,kwani watu hao wamekuwa wakikusanya fedha zisozo katika mpangilio na kusababisha taharuki’’amesema.

Akijibu hoja hizo mbele ya kikao,Afisa wa sharia kutoka mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini kutoka makao makuu Dodoma,Martha Ngaga,amesema hakuna sharia inayoruhusu mbia wa kukatisha Leseni kuendesha msako.

Amesema mkataba wake na Latra ni kukatisha Leseni tena awe kwenye ofisi yake inayotambuliwa na sio kuzunguka mitaani kufanya msako,na pia amesema kosa lingine ni kutumia nembo ya Latra kuzunguka mitaani kukusanya fedha huku akipiga marufuku mfumo huo.

Katika semina hiyo,Irene Sawe afisa sharia wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA) mkoani Songwe,amesema serikali imeweka wazi mipango mizuri na ndiyo maana wamekuwa wakiwafikia pale walipo kuwakumbusha madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuzijua sharia.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa