Wananchi watakiwa kushiriki miradi ya maendeleo





Na Asha Hassan,Nkasi
‎Vongozi wa kata ya Isale Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa akiwemo Diwani wametakiwa kwenda kuwahamasisha wakazi wa kijiji cha Mtapenda kata ya Isale kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mradi wa vyoo wa SWASH unaotekelezwa katika Shule ya Msingi Kitete.
‎Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Ufundi Optunatus Mussi kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi katika kikao cha maendeleo ya kata kilichofanyika katika Ofisi ya Kata ya Isale mara baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya mradi huo ambao utagharimu kiasi Cha Shilingi Milioni thelathini na nne sitini elfu miatisa na hamsini na moja na senti kumi na tatu.

Aidha Mussi amewasisitiza kuwa wao kama viongozi wanatakiwa kutumia utashi na kukubalika kwao kwa wananchi kuendelea kuwasawishi wakazi hao kushiriki ujenzi wa mradi huo kwa nguvu zao kama Sheria ya mradi inavyosema, kwani serikali ina dhamira ya dhati ya kusogeza huduma ya Elimu kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Renatus Danda akizungumza katika kikao hicho amesema kuwa kupitia viongozi hao wananchi wanatakiwa kufahamishwa kuwa miradi hiyo ya SWASH, nguvu za wananchi zinahitajika moja kwa moja ambapo changamoto kubwa kwa mujibu wa taarifa ya maendeleo ya mradi wananchi hawashiriki kwasababu Shule hiyo iko kwenye eneo la magereza hivyo wao wanaona kama haiwahusu ilhali Shule hiyo ni Mali ya wananchi.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa