KUKAMILIKA KWA BARABARA YA KAPELE-NDARAMBO KWAWAFURAHISHA WANANCHI
Na Ibrahim Yassin,Songwe.
Ukarabati wa barabara ya Kakozi_Ilonga enye urefu wa kilomita 49.6 Imeelezwa kuondoa adha kwa wananchi wa kata ya Kapele na Ndalambo wilayani Momba mkoani Songwe kutumia siku 5 mpaka 7 njiani kwenda katika wa Tunduma.
Ukarabati kwa barabara hiyo umekuja baada ya kupandishwa hadhi na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania(TANROAD) Mkoa wa Songwe kutoka Wakala wa barabara za mijini na vijijini(Tarura).
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti leo April 3/2024 baadhi ya wananchi wamesema barabara hiyo ilikuwa kero kiuchumi lakini kwa sasa imekuwa chachu ya maendeleo kwani inawafikisha maeneo muhimu ikiwemo mji wa Tunduma..
Mkazi wa kijiji cha Kakozi Godi Mtambo , amesema awali walikuwa wanatumia siku 5 mpaka 7 kufika Tunduma kutokana na ubovu wa barabara iliyokuwa ikiasababisha magari kukwama njiani wakisaka mahitaji muhimu.
"Barabara hii imekuwa mkombozi wakulima wengi wa Kata za Kapele na Ndalambo wameanza kunufaika kwa kusafirisha mazao ”amesema.
Neya Agnesi Sichalwe amesema wafanyabiashara walikuwa wanashindwa kufika kununua mazao wakihofia kukwama kwa magari yao ,hali ambayo ilipelekea uchumi wa wananchi kushuka.
Mtendaji wa kijiji cha Kakozi Maria Maketta amesema kuboreshwa kwa barabara hiyo itafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Sumbawanga vijijini na nchi jirani ya Zambia kupitia Wilaya ya Momba.
Diwani wa Kata ya Ndalambo Fravian Sichizya amesema awali barabara hiyo ilikuwa inasimamiwa Tarura lakini kwa sasa imepandishwa hadhi na kusimamiwa na Tanroad Mkoa wa Songwe ambao wameanza mchakato wa kuboresha.
Sichizya amesema awali barabara hiyo haikuwa inapitika mwaka mzima na kuleta adha kwa wananchi kusafirisha mazao yao kama Mahindi,Mpunga, Karanga na Mtama ambao ndio kitega uchumi chao kikubwa.
"Serikali inatakiwa kuiweka kwenye bajeti barabara hiyo ijengwe kwa kiwango cha rami ili kukuza uchumi wa wananchi na nchi Jirani ya Zambia kusafirisha mazao .
Kwa upande wake Meneja wa Wakala Barabara Tanzania Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amesema kabla ya kupandishwa hadhi barabara hiyo wananchi walikuwa wanashindwa kusafirisha mazao kutoka nchi jirani ya zambia eneo la Kasesa na wananchi wa wilaya ya Momba na Rukwa wilaya ya Sumbawanga vijijini.
"Licha ya kukarabati barabara hiyo Kuna maeneo korofi ambayo kwa sasa wakandarasi wapo eneo la kazi kurekebisha na kuhakikisha yanapitia wotena kukuza uchumi kwa wananchi wanaotegemea kilimo kusafirisha mazao yao," amesema mhandisi Bishanga.
Katika hatua nyingine Mhandisi Bishanga amesema wakala wa Barabara Tanzania mkoa wa Songwe kwa miaka mitatu ya Rais Samia kuwa madarakani wamepokeza fedha zaidi ya Sh .170 bilioni amabazo zimetumika kwenye matengenezo ya Barbara kuu, mkoa na madaraja likiwepo daraja la mto Momba



Comments
Post a Comment