MABARAZA YA KATA YAPIGWA 'STOP'KUTOA HUKUMU YAJIKITE KWENYE USULUHISHI
KAIMU mkuu wa wilaya Nkasi ambaye pia ni mkuu wa wilaya Kalambo mkoani Rukwa Razaro komba amepiga marufuku kwa mabaraza ya ardhi ya kata kutoa hukumu badala yake yajikite kwenye usuluhishi ili kuweza kuleta utengamano katika jamii.
Agizo hilo amelitoa jana wilayani Nkasi kwenye mkutano wa Wadau kujadili mradi wa utekelezaji wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi wilayani Nkasi ambapo amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha mabaraza hayo lilikua ni zuri kinyume chake yamekua chanzo cha kukuza migogoro.
Amesema kuwa mabaraza hayo yalipewa dhamana ya kusikiliza kesi na kutoa maamuzi lakini mwaka 2021 serikali ilibaini udhaifu kwenye mabaraza hayo na kuyaondolea nguvu ya kutoa maamuzi na badala yake yajikite kwenye usuluhishi pekee.
Kufuati hari hiyo ameiagiza halmashauri ya wilaya kupitia kupitia kitengo chake cha sheria kufikia ijumaa ya wiki hii iwe imetoa mafuzo kwa wenyeviti ,makatibu na wajumbe wote wa mabaraza ya kata kuwajengea uwezo wa kisheria namna ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi inayofikishwa katika mabaraza yao.
Kaimu mkuu huyo wa wilaya amedai kuwa ardhi ina mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo ni lazima ardhi ikatengenezewa utaratibu madhubuti wa kuilinda na kuwa mradi huo wa uboreshaji wa usalama wa miliki za za ardhi ni suluhisho la tatizo hilo .
Alidai kuwa mradi huo ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano ni lazima wahakikishe kuwa unaleta tija na miliki zitakazopatikana ziwasaidie Wananchi katika kujiletea maendeleo katika Nyanja mbalimbali kwani ardhi inagusa kila sekta.
Meneja msaidizi wa mradi huo toka makao ardhi Patrick Mwakilili alidai kuwa wao watahakikisha mradi huo wa( LTIP) unawafikia Wanananchi wote na kuona changamoto katika sekta hiyo ya ardhi inapungua kwa kiasi kikubwa hasa baada ya mpango wa matumizi sahihi ya ardhi utakapokamilika
Meneja huduma kwa wateja wa Bank ya NMB wilayani Nkasi Marijani James alidai kuwa mradi huo wa usalama wa miliki ardhi una fursa pia kwao kwa maana wataweza kutoa mikopo zaidi kwa Wananchi ikiwemo mikopo ya kilimo na ufugaji yenye riba ndogo sana ukilinganisha na mikopo ya aina nyingine.
Alifafanua kuwa mikopo ya kilimo na mifugo utozwa riba ya 9% ukilinganisha na riba ya mikopo ya biashara riba ni 21% na mingine riba 23% na kuwa kwa mwaka jana tu wa 2023 wameweza kutoa mikopo ya Bil.4 kwa Wakulima na wafugaji wa wilaya Nkasi na kuwa mpango huo wa urasimishaji ardhi kupitia mrati wa uboreshaji usalama wa miliki wa ardhi (LTIP) utawasaidia watu wengi ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha kuweza kutoa mikopo mingi kwa jamii na kujikwamua kiuchumi
Mwisho



Comments
Post a Comment