Mbunge ashiriki kula Pasaka na Wananchi wake



Na Israel Mwaisaka,Nkasi

MBUNGE wa jimbo la Nkasi kusini mkoani Rukwa Vicent Mbogo ameisherehekea sikukuu ya Pasaka kwa kula pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kata ya Chala pamoja na Wananchi na kuutumia muda huo kukusanya mawazo kutoka kwao ambayo atakwenda kuyapeleka bungeni.

Akizungumza na viongozi hao Mbogo alidai kuwa ameamua kuwakutanisha katika sikukuu hiyo ya Pasaka ili waweze kula pamoja na kuwapa nafasi wao ya kumweleza mambo ya msingi ambayo wao wanaona kuwa yana umuhimu kwenda kuzungumzwa kwenye vikao vya Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa kuna wakati ni ngumu kwa watu kuweza kukutana na Mbunge na kumweleza mambo ya msingi na kwa kuona hilo ameamua kuitumia sikukuu ya Pasaka ili kuweza kula na kunywa pamoja na kuwa hiyo inawarahishia Wananchi kuweza kuzungumza mambo ambayo wanafikiri yanaweza kuzungumzwa na kupewa kipaumbele na mwakilishi wao katika utekelezaji

Mwenyekiti wa CCM kata ya Chala Johakimu Mwakampya aliwataka Wajumbe wa mkutano huo kuitumia nafasi hiyo kueleza mambo ya msingi ili Mbunge wao aweze kuyachukua na kwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya maendeleo yao.

Alifurahishwa na kitendo cha Mbunge wao kuwaita na kula nao sikukuu ya Pasaka na kuwa jambo hilo limewafanya wawe wamoja ikiwa ni pamoja na kila mmoja wao kuweza kumfikia Mbunge wao kiurahisi na kuweza kueleza mambo yao yaliyopo moyoni.

Baadhi ya Wananchi hao Emmanuel Masunga,Albenia Msonje na Ernest Ulaya walimweleza Mbunge kuwa wao wanataka miradi inayotekelezwa katika jimbo la Nkasi kusini yaendane sawa na gharama za mradi na kumuomba Mbung wao awe macho kwa watendaji wanaotekeleza miradi hiyo kwa kuwafuatilia ili miradi itekelezwa sawa na thamani husika ya fedha zilizotolewa na serikali.
sawa na gharama za mradi na kumuomba Mbung wao awe macho kwa watendaji wanaotekeleza miradi hiyo kwa kuwafuatilia ili miradi itekelezwa sawa na thamani husika ya fedha zilizotolewa na serikali.




Diwani wa kata ya Chala Michael Mwanalinze alimpongeza Mbogo kwa namna anavyowawakilisha bungeni na jimbo hilo kuweza kuwa na miradi mingi ya maendeleo na kuwa na wao kama viongozi wa chini yake wanahakikisha kuwa wanamsaidia katika kusimamia miradi hiyo ya maendeleo

Pia alitumia nafasi hiyo kumweleza Mbunge kuwa asiwe na wasiwasi na asipende kupokea maneno kutoka kwa Watu yenye lengo la kuwachonganisha na kuwa huu ni wakati wa kuwa pamoja na kushikamana ili kile walichowaahidi Wananchi kiweze kutekelezeka na wakakiona

Awali katibu kata wa kata hiyo Edwini Mwanakulya alimtaka Mbunge kuendelea kufanya hivyo kwa kuwakutanisha Wananchi na kuweza kuzungumza mambo yao kwa uwazi badala ya kila mtu kumtafuta kwa wakati wake kitu ambacho kinaleta usumbufu


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa