WAWILI WAFARIKI BAADA YA MLIMA KUMEGUKA NA KUFUNIKWA NA TOPE

Na Israel Mwaisaka,Sumbawanga

MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa zimesababisha kupasuka kwa kipande cha mlilima wa lyambalyamfiopa katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya sumbawanga na kusababisha watu wawili wa familia moja kufariki dunia katika kitongoji cha Kamoko kata ya Muze baada ya kufukiwa na tope zito lilitokana na maporoko ya maji huku nyumba 38 zikianguka katika kata ya kapenta.

Wakazi wa kijiji hicho katika nyakati tofauti wamesema licha ya hilo mvua hiyo imeharibu mazao na baadhi ya nyumba kuharibiwa na watu 15 kujeruhiwa.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha uzia dkt maiko mwaipora amesema amewapokea watu 15 walikuwa wamejeruhiwa na watu wawili wakiwa wamefariki dunia na kuelezea hali za wagonjwa.

Hata hivyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo imetembelea maeneo hayo, ambapo mkuu wa wilaya ya sumbawanga nyakia chirukile,amewataja waliofariki duinia kuwa ni Sai Weja ( 26) na Geshi Gwesu mwenye umri wa miaka 7 wote wakazi wa kijiji cha Uzia.

Aidha amesema licha ya hilo nyumba 38 zimeanguka katika kata ya Kapenta kutoka na mvua hizo.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa