WATOTO 32,168 NKASI KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA UZAZA (HPV)
Na Israel Mwaisaka,Rukwa
WILAYA ya Nkasi mkoani Rukwa inatarajia kuwachanja Watoto wa kike wapatao 32,168 kukabiliana na maradhi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi
Akizindua chanjo hiyo katika shule ya msingi ya Isunta kaimu mkuu wa wilaya ya Nkasi na ambaye pia ni mkuu wa wilaya Kalambo Razaro Komba amewataka wanananchi kuhamasika na kuhakikisha watoto wao wote waliofikisha umri wa miaka 9 hadi 14 wanaipata chanjo hiyo.
Alidai kuwa zoezi hilo la chanjo ambalo litadumu kwa muda wa siku 5 litakua na maana sana kama walengwa wote wataipata chanjo hiyo ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo wa saratani ya shingo ya uzazi ambalo kwa sasa limekuwa ni tatizo kubwa na limeleta athari katika jamii.
Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuwa chanjo hiyo imeanza kutolewa toka mwaka 2014 mkoani Kilimanjaro na mpaka sasa imedumu kwa muda wa miaka 8 na serikali imeendelea kuitoa chanjo hiyo kutokana na changamoto wanayoipata Wanawake hasa pale wanapokumbwa na ugonjwa huo.
Hivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji kuhakikisha kuwawanatoa hamasa ya kutoshas kwa watu wanaowaongoza kuhakikisha watoto wao wote wanapata chanjo hiyo.
Awali kaimu mkurugenzi mtendaji wa wilaya Ladislaus Mzelela alisema kuwa licha ya chanjo hiyo kutolewa katika shule zote lakini pia vituo 59 vimeandaliwa kwa ajili ya kutolea chanjo hiyo ya HPV katika wilaya Nkasi.
Alidai kuwa ana uhakika kuwa Watu wengi watajitokeza kupeleka Watoto wao ili kuweza kupata chanjo hiyo kutokana na hamasa kubwa ambayo imeendelea kutolewa katika maenero mbalimbali ya wilaya Nkasi.
Diwani wa kata ya Isunta Aizeck Chambula amesema kuwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi unajulikana sana katika jamii na wengi wamewapoteza ndugu zao kutokana na ugonjwa huo na kuwa hatashangaa kama watu hao watashindwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chanjo hiyo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Isunta Chrispini Wikula alimuhakikishia mkuu wa wilaya kuwa wao kama viongozi watahakikisha watu wote katika maeneo yao wanawapeleka Watoto watoto wao wote kupata chanjo ili ili kuweza kuwaweka Watoto wao katika mazingira salama.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa chanjo hiyo ya HPV wamesema kwamba wao wanatambua umuhimu wa chanjo hiyo na madhara yatokanayo na ugonjwa huo hivyo hawaoni sababu ya kutowapeleka watoto wao kwenda kupata chanjo hiyo




Comments
Post a Comment