Na Israel Mwaisaka, Nkasi Salum Kazukamwe na Moses Kaegele wameshinda katika Kura za maoni za kuwania Ubunge katika Majimbo mawili ya Nkasi Kaskazini na kusini yanayounda wilaya Nkasi Akitoa taarifa juu ya zoezi zima la upigaji wa Kura za maoni lililofanyika Jana katibu wa CCM wilaya Nkasi Anastazia Almasi amesema kuwa wilaya Nkasi inaundwa na Majimbo mawili ya Uchaguzi na makada 10 wa CCM walifanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho na wawili hao kupenya kuweza kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.. Amesema kuwa kwa upande wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Salumu Kazukamwe ameshinda kwa kupata Kura 2956 akifuatiwa na John Sichilima aliyepata kura 1471, Jonas Kifunda 560, Thomas Kalunga kura 320 na wa mwisho Ni David Siame aliyeambulia 137. Kwa upande wa Jimbo la Nkasi kusini Moses Kaegele ameshinda kwa kupata Kura 3028 akifuatiwa na Vicent Mbogo aliyepata 1,623, Evarist Christopher Mwanansao Kura 465,Desderius Mipata Ku...
Comments
Post a Comment