Vikundi 200 Vya Wanufaika Wa TASAF Kuanzishwa Wilayani Kalambo


Wanufaka wa mradi wa TASAF wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vitakavyo wawezesha kukuza uchumi wa kaya kwa kuanzisha miradi ya pamoja na kupata mikopo itakayo wawezesha kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa TASAF wilayani humo Mariam Kimashi wakati wa kampeni ya uundwaji wa vikundi kwenye vijiji vya kata za Matai na Lyowa.
amesema kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa vikundi, Halmashauri imeanzisha mpango wa kuwaunganisha wanufaika kwenye vikundi na kwamba wanatarajia kuunda vikundi 200 ambapo kila kikundi kitakuwa na wanufaika 15.

lengo la serikali ni kuwaweka pamoja wanakikundi ili kuongeza uchumi wa kaya na kwamba endapo kikundi kitafanya vizuri na kuwa na uwezo basi TASAF itakipatia ruzuku ya uzalishaji ili kuifanya kaya kujikwamua kiuchumi’’alisema KimashiHata hivyo baadhi ya wanufaika wa TASAF wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuwawezesha kifedha na kwamba kuanzishwa kwa vikundi hivyo kutaenda kuwaondolea adha ya kuwa tegemezi katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa