Watatu mbaroni kwa mauaji ya mfanyabiashara na kumpora mali




Na Israel Mwaisaka,
Sumbawanga

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia wanaume watatu wakazi wa Kijiji cha Katazi wilayani Kalambo mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga rungu kisha kumzika akiwa hai mfanyabiashara wa mazao Baraka Nyangala(30) lengo likiwa ni kupora fedha alizo kua ameenda kununulia mazao.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Oktoba 16 ambako alikwenda kununua Maharagwe akiwa na watu walio muua.

Inaidawa kuwa mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawangaa alipigiwa simu na watuhumiwa ambao ni Frank Simsokwe (33), Edfonsi Simsokwe (28) ambao ni mkubwa na mdogo pamoja na Nikas Lunguya (38) kuwa wanamaharage hivyo walimuita ili aende akanunue.

Baada ya marehemu kufika kijijini hapo wakatumia usafiri wa usafiri wa pikipiki wakidai kuwa wanampelekea sehemu yalipo maharage hayo na walipofika maeneo ya porini walimtaka mfanyabiashara huyo asimamishe pikipiki yake.

"Baada ya kusimamisha pikipiki hiyo mmoja kati ya watuhumiwa hao alimpiga kwa rungu kichwani mfanyabiashara huyo kisha kupoteza fahamu na kumpora fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 1, 840,000 pamoja na pikipiki" alisema Kamanda Masija.

Kamanda huyo alisema baada ya kumjeruhi na rungu kichwani na kuona kuwa amepoteza fahamu waliamua kuchimba shimo kisha kumfukia mfanyabiashara huyo akiwa bado yupo hai na wao kutokomea kusikojulikana.

Alisema baada ya kutoweka ghafla kwa mfanyabiashara huyo, ndugu wa marehemu walitoa taarifa Polisi ambapo kwa kutumia interejensia na wataalamu wa Cyber crime walifanikiwa kuwakamata watu hao.

ACP Masija alisema watuhumiwa hao waliwaongoza hadi eneo ambalo waliufukia mwili wa marehemu na ulifukuliwa kwa uchunguzi na taratibu nyingine za kuukabidhi mwili huo kwa ndugu zao kwa ajili ya maziko.

Kamanda alisema kuwa watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa