Ukarabati wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga wafikia asilimia 96



Na Israel Mwaisaka,Rukwa
‎Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Mwakiposa Kihenzile, ametoa wito kwa sekta binafsi na makampuni ya ndege kuwekeza katika huduma za usafiri wa anga.
‎ Kihenzile ametoa wito huo Jana Februari 21, 2026 akiwa mkoani Rukwa, ambapo amekagua hatua mbalimbali za maendeleo ya ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga.
‎Naibu Waziri huyo alieleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege ili kuimarisha miundombinu ya sekta hiyo.
‎Aidha ameeleza kuwa wito huo unalenga kupunguza changamoto zilizopo na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi na wawekezaji.
‎Akitoa taarifa ya maendeleo ya kazi ya ukarabati, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa na msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Joseph Jemonge, amebainisha kuwa kiwanja hicho kimefikia asilimia 96 ya ukamilishaji, huku kazi zilizobaki zikihusisha hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika rasmi.
‎Naibu Waziri pKihenzile amesisitiza umuhimu wa kukamilika kwa wakati kwa kazi zilizobakia ili kiwanja kianze kutoa huduma.
‎Wananchi na viongozi wa Mkoa wa Rukwa waliohudhuria wamepongeza hatua za ujenzi zilizofikiwa, wakieleza matumaini yao ya kuanza kutumika kwa kiwanja hicho hivi karibuni.
‎Mradi huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za biashara katika Mkoa wa Rukwa.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa