Madiwani Nkasi watakiwa kubadilika baada ya mafunzo
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
MADIWANI wametakiwa kubadilika kwa kufanya kazi kisasa baada ya kupata mafunzo ya kiuongozi yaliyotolewa na chuo Cha Serikali za mitaa Hombolo.
Hayo yamesemwa leo Februari 21,2026 na Mwakilishi wa Katibu tawala wa mkoa Rukwa Vaileth Shirima alipokuwa akifunga mafunzo ya tatu kwa Madiwani wa halmashauri ya Wilaya Nkasi.
Amesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yakawaimarishe kiutendaji na kuwa wapya kwa kuongeza nguvu katika kuwahudumia Wananchi waliowachagua.
Alidai kuwa Madiwani wapya ni wengi ukilinganisha na waliorudi katika awamu hii nyingine hivyo anatarajia kuona wote wanajua wamoja na kuhakikisha majukumu Yao hayaingiliani na ya Watu wengine ili kuondoa migongano inayoweza kuzalisha migogoro isiyokuwa ya lazima.
Mashaka Makuka afisa tawala mwandamizi OWM-TAMISEMkwa upande wake amesema kuwa Imani yake ni kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yatakwenda kuibadili halmashauri kwa kuiwezesha kuwa bora zaidi na Kutoa huduma stahiki kwa Wananchi.
Alidai kuwa Udiwani si cheo Cha heshima tu bali wanalo jukumu kubwa zaidi hasa pale wanapokuwa na mawazo chanya katika kuiendeleza halmashauri Yao.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri Richard Maasai alidai kuwa Madiwani wanalo jukumu kubwa la kulinda rasilimali za halmashauri nje ya jukumu kubwa walilonalo la usimamizi wa Watumishi wa halmashauri.
Alifafanua kuwa ni jukumu la Kila mmoja kuhakikisha kwamba rasilimali za halmashauri zinatunzwa na kulindwa ipasavyo ili ziweze kuwanufaisha Wananchi badala ya kung'ang'ana na jukumu moja tu la kuwasimamia Watumishi.
Awali kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya Nkasi Vareliana Mwampasi aliwaomba Madiwani kuchukuliana na watendaji wao wa Serikali na kujenga umoja na maelewano yatakayowasaidia kutekeleza majukumu Yao vyema .
Madiwani kwa upande wao wamehaidi kuyatumia mafunzo hayo kuwaimarisha kiutendaji na kuyajua majukumu Yao sawa sawa .





Comments
Post a Comment