Bodaboda Nkasi wakabidhiwa refrector za Takukuru kuchagiza mapambano dhidi ya rushwa
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Katika jitihada za kupambana na vitendo rushwa taasisi ya Kuzuia na Kupambana rushwa (TAKUKURU) wilayani Nkasi mkoani Rukwa imekabidhi reflector kwa Madereva wa Bodaboda zenye ujumbe mahususi juu rushwa.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo afisa Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU wa Wilaya Nkasi Fauzi Mponda amesema kuwa wameamua kukabidhi reflector hizo kama njia mojawapo ya kufikisha ujumbe kwa jamii na kueleza ubaya wa vitendo vya rushwa katika jamii.
Amesema kuwa Bodaboda ni moja ya kundi kubwa katika jamii na kwamba na wao ni moja ya washawishiwa Kutoa rushwa hivyo ujumbe uliopo kwenye reflector hizo utapelekea kukumbuka kuwa nao wapo kwenye mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu wa Wilaya Nkasi Peter Lijualikali kwa upande wake amewataka Bodaboda hao wakawe mabalozi wema katika vita hiyo dhidi ya rushwa na kuwa mstari wa mbele kukataa vitengo vyoyote vya rushwa iwe ni Kutoa Wala kutokea rushwa.
Amesema kuwa rushwa ina madhara makubwa katika jamii na kuwataka kuwa karibu zaidi na taasisi ya kupambana na Kuzuia rushwa ili kuweza kukabiliana na mbinu mbalimbali za rushwa za kuukwepa mkono wa sheria.
Mwenyekiti wa umoja wa Bodaboda wilayani Nkasi Alfred Matofali kwa upande wake amewashukuru TAKUKURU kwa kuwakumbuka na kuwa na wao watajitahidi Kutoa ushirikiano wa dhati katika kuwaumbua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya rushwa.
Amesema kuwa rushwa madhara yake ni makubwa na wengi wanayafahamu hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanashirikiana na Takukuru katika kuwabaini,kuwafichua ikiwa ni pamoja na Kuzuia mianya yoyote ya rushwa wanayoifahamu.




Comments
Post a Comment