NKASI YAJIPANGA NA MASHINDANO YA LIGI YA WANAWAKE DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Wilaya Nkasi mkoani Rukwa inajiandaa kuwa mwenyeji wa mshindano ya mpira wa miguu kwa Wanawake ligi daraja la tatu huku maandalizi yakiwa hatua za mwisho.
Akizungumza na Majira katibu wa chama cha mpira wa miguu wilayani Nkasi (NFA) Michael Charahani amedai kuwa mashindano hayo yanatarajia kuanza mwezi Marchi ya mwaka huu.
alisema kuwa wilaya Nkasi ambayo inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano hayo itapeleka timu tatu ambazo ni Nkasi Queens, Chala Princess na Kirando Queens.
Charahani amedai kuwa wao kama wenyeji wa mashindano hayo wamekamilisha karibia maandalizi yote na viwanja viwili vinatarajia kutumika katika mashindano hayo.
amevitaja viwanja hivyo kuwa ni uwanja wa Sabasaba mjini Namanyere ikiwa ni pamoja na uwanja wa shule ya sekondari Nkasi na kuwa Sumbawanga Manispaa na wilaya ya Kalambo zinatarajia kupeleka timu zao wilayani Nkasi ili kuweza kushiriki mashindano hayo.
katibu huyo wa NFA amefafanua kuwa licha ya maandalizi hayo kukamilika lakini changamoto kubwa waliyonayo ni ukata baada ya kushindwa kupata wafadhili wa mashindano hayo.
"" Ufadhili kwa ligi na timu zetu ni mdogo sana kiasi cha kupelekea kushiriki ligi hiyo katika mazingira magumu"" alisema Charahani
washindi watakaopatikana katika ligi hiyo watakwenda kushiriki ligi daraja la pili ambapo TFF wataandaa kituo cha mashindano hayo.
Mwisho

Comments
Post a Comment