Wapiga kura uchaguzi mkuu Nkasi watangaziwa rasmi siku ya kupiga kura
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
Tume huru ya taifa ya Uchaguzi Jimbo la Nkasi Kaskazini na Nkasi kusini kwa mujibu wa kifungu Cha 69 (1)1 imetangaza rasmi Kuwa Oktoba 29,2025 Ni siku ya kupiga Kura kwa wale wote waliojiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga Kura.
Akitoa tangazo hilo leo Oktoba 20,2025 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini na Nkasi kusini George Mwahinda amesema kuwa vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga Kura ndivyo vitakavyotumika kupigia Kura.
Amesema kuwa pamoja na tangazo hilo katika kila kituo cha kupigia Kura zimebandikwa taarifa mbalimbali ikiwemo karatasi ya mfano yenye majina na picha za kila mgombea pamoja na Nembo ya vyama vyao vya siasa kwa Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani.
Pia nitakuwepo na orodha ya majina ya Wapiga Kura walioandikishwa na tume huru ya taifa ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na orodha ya Wapiga kura walioruhusiwa kupiga Kura moja tu ya Rais
Mwahinda amefafanua kuwa vituo vyote vya kupigia Kura siku ya Uchaguzi vitafunguliwa saa 1:00 na kufungwa saa 10:00 za jioni na kwa upande wa vituo vya kupigia Kura vya Magereza vitafunguliwa saa 2:00 za asubuhi na kufungwa saa 9:00 alasiri.
Hivyo katika kipindi hiki Wananchi wote wanatakiwa kupitia taarifa hizo zilizowekwa katika vituo Ili kuweza kutambua mapema vituo watakavyopigia Kura na kuona mfano wa karatasi ya Kura.
Mwahinda ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi katika Majimbo yote mawili amesema kuwa katika Majimbo yote mawili wanatarajia watakaopiga Kura ni 214,219 ambapo Nkasi Kaskazini Ni 125,078 na kusini Ni 8,9141


Comments
Post a Comment