SONGWE DC -YAJIVUNIA KUKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME NGAZI YA VIJIJI IKIKARIBIA KUKAMILISHA VITONGOJINI
- Get link
- X
- Other Apps
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANANCHI katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe,wameupongeza uongozi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) wilayani humo kwa kukamilisha kikamilifu usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote.
Wilaya ya Songwe yenye vijiji 43 ikiwa na vitongoji 205 na jimbo moja la uchaguzi huku makao makuu ya wilaya yakiwa katika kata ya Mkwajuni imefikia hatua nzuri ya kukamilisha vitongoji vyote usambazaji umeme katika miezi mitatu ijao.
Licha ya upya wake wilaya hiyo iliyomegwa kutoka wilaya ya Chunya mkoani Mbeya miaka kumi iliyopita ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhba wa nishati ya umeme lakini katika utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu,wamefanikiwa kusambaza umeme vijiji vyote 43.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 27/2025 na meneja wa shirika hilo wilayani Songwe Mhandisi Michael Kidoto wakati akizungumza na dira kamilifu ofisini kwake na kusema wilaya ina vijiji 43 vyote vinahuduma za umeme na sasa wamehamia kukamilisha usambazaji huo kwenye vitongoji.
Amesema katika wilaya nzima yenye vitongoji 205 kati ya hivyo vitongoji 145 vimesambaziwa umeme ambapo 60 vilivyosalia kati ya hivyo vitongoji 40 vipo katika hatua za mwisho ambapo ndani ya miezi 3 vitawashiwa umeme.
Ameongeza kuwa vitongoji vitakavyosalia ni 175 ambapo tayari vifaa vimeletwa tayari kwa ukamilishaji na kuwa wamejipanga kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa na umeme kila kitongoji hali itakayozalisha uchumi kutokana na shughuri za kibiashara zitakazotegemea umeme.
Ameongeza kuwa shughuri hizo za usmbazaji umeme zinafanywa na kampuni mbili ambazo ni CDCEBG na JV-MF and Gassap electrocal and Electronic Co ambazo zinafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha zinakamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Aneth Chilewa mkazi wa Mkwajuni amesema tangu umeme kusambazwa katika eneo lote la Mkwajuni uchumi umekuwa kwa kasi kutokana na watu kufungua salooni,mashine za kusaga na hata taasisi kubwa na kuufanya mji wa mkwajuni na maeneo mengine kuwa kama Dar es salaam ndogo.
Jimmy Mwashilindi mkazi wa Gua amesema uwepo wa umeme umesababisha hata mitandao ya simu kusambazwa eneo hilo na kuwa wajasiliamali kutoka ndani nan je ya eneo hilo wamefika kufungua shughuri za kiuchumi hali iliyoondoa lindi la umasikini kwa jamii.






Comments
Post a Comment