NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA SPEEDI YA WAKANDARASI WANAWAKE
- Get link
- X
- Other Apps
Wizara ya ujenzi chini ya wakala wa barabara mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Songwe imetii agizo la Serikali la kuwpatia wakandarasi wanawake wazawa kujenga barabara za Lami ambapo ilitoa tenda ya ujenzi wa kilometa 20 zinazogharimu Tsh,Bilioni 45.447.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika kujenga barabara ya Ruanda-Idiwili yenye thamani ya Bilioni 45.447 yenye kilometa 20 ambapo kilometa 5 zimetolewa kwa wakandarasi wanne watakaojenga kilometa tano tano ambapo jana walisaini mikataba ya utekelezaji wa mradi huo
Baada ya wakandarasi wa kampuni hizo nne kuanza ujenzi mkoani Songwe,Naibu katibu mkuu Dkt,Msonde,mwishoni mwa wiki alifika kuikagua miradi hiyo huku akiridhishwa jinsi wanawake hao walivyoanza vyema ujenzi huo..
Katika ziara yake alianzia wilayani Ileje ambako alikagua ujenzi wa barabara na madaraja likiwemo daraja la Bilioni 7.942 linalotarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi kwa kufungua fursa za kiuchumi katika usafirishaji wa mazao.
Na pia siku hiyo hiyo alipata wasaha wa kuzitembelea barabara zilizo katika matengenezo ambazo ni barabara ya Ruanda-Nyimbili-Hasamba-
Mradi huu wa barabara ya Ruanda-Idiwili-kwa kiwango cha Lami yenye urefu wa kilometa 20 ni moja ya barabara ya mikakati ya serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani Songwe.
Ujenzi wa barabara hii umefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya ujenzi kupitia wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) ambaye ndiye mwangalizi mkuu wa mradi.
Hata hivyo ujenzi wa barabara hizo unafanyika kwa viwango vya upana wa mita 11,ambapo mita 7.0 ni njia ya magari na mita 2.0 kila upande ni upana wa mabega ya barabara kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.
Meneja wa wakala wa barabara Mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Song we,Mhandisi Suleiman Bishanga alimueleza Naibu katibu mkuu huyo kuwa wapo bega kwa began a wakandarasi hao kuhakikisha ujenzi unajengwa na kukamilika kwa obora wa viwango vya juu.
Katika ukaguzi huo Naibu katibu mkuu alisikiliza risala ya viongozi wa kampuni hizo ambapo moja ya ombi lao ni kupatiwa malipo haraka ya kazi zilizofanyika ili waendelee kujenga kwa kasi na kumaliza kwa wakati mradi huo kama mkataba unavyotaka.
Rais wa wakandarasi wanawake wazawa Judith Odunga alisema kuwa wapo tayari kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kutii agizo la Serikali la kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Alisema wamefikia hatua nzuri ya ujenzi,kazi iliyopo kwa sasa ili waongeze kasi wanaomba waongezewe fedha na kuwa wanauhakika hawataiangusha serikali katika ujenzi wa mradi huo.
Deborah Sengati, mkurugenzi mtendaji kampuni ya ULM alisema wana kila sababu ya kuipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha wanawake wazawa kufanya kazi za ujenzi wa miradi ya barabara,na kuwa watahakikisha wanajenga kwa kufuata viwango bora.
Dkt,Msonde baada ya kusikiliza Risala na maelezo ya viongozi wa kampuni hizo,alisema sera ya nchi kwa sasa inahitaji wakandarasi wa ndani hasa wanawake wajenge barabara na madaraja ambapo kwa kuanzia walianza kutoa miradi ya Bilioni 10 na wameridhishwa na kasi ya ujenzi.
‘’Wizara ya ujenzi ndiyo wasimamizi wenu wakuu,nimekuja hapa kujionea jinsi ujenzi unaofanywa na wakandarasi wanawake wazawa wa kampuni 4 unavyoenda,nime ridhishwa na kazi ya ujenzi’’alisema Dkt,Msonde.
Aidha Dkt,Msonde aliwaeleza viongozi hao wa kampuni hizo nne,kuwa wapo kuwaandalia nyongeza ya fedha za mradi huo ili waendeleze kasi ya ujenzi huku akisema mpango uliopo ni kuwaongezea uwezo wa kujenga miradi mikubwa zaidi.
Aliongeza kuwa kwa sasa wanajiandaa kupendekeza kila kampuni iweze kupata mradi wa Bilioni 50 ukilinganisha na awali walivyowapitishia uwezo wa kujenga miradi isiyozidi Bilioni 10 kwa kampuni moja.
Sehemu ya kwanza ya ya ujenzi kilometa 5 zinajengwa na mkandarasi wa kampuni ya M/s ULM Investment na HIGO Investment pamoja na TANZH ON Limited JV za jijini Dar es salaam kwa kiasi cha Tsh,11,744,575,894.07 ( Bil,11.745).
Sehemu ya pili kilometa 5 zingine zinajengwa na mkandarasi M/s AB Msengi & Hysten & M/s MSETTI Women Contractor JV wa jijini Mbeya kwa gharama ya Tsh,10,485,464,,175.03 (Bil,10.458).
Sehemu ya tatu ya mradi huo kilometa 5 zinajengwa na mkandarasi M/s Ibra Contractors limited,M/s Nail IT Construction Limited na M/s Kimango Engineering Company limited JV wa jijini Dar es Salaam kwa Tsh,12,464,651,295.28 (Bil,12.465.
Sehemu ya nne nayo ni kilometa 5 zinajengwa na mkandarasi M/s JUDEX Contractor Limited,M/s Cyfloa 2020 Company limited na M/s ML Smart Company limited JV za jijini Dar es Salaam kwa gharama ya Tsh,10,752,024,122.83,(Bil,10.
Maida Waziri mkandarasi wa kampuni ya Ibra Contrctor alisema anakila sababu ya kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kukitambua chama cha makandarasi wanawake Tanzania (TWCA) kwa kuwezeshwa kupatiwa miradi.
Alisema baada ya kuona kazi zote za ujenzi wanapewa wakandarasi wanau me walianzisha umoja wa makandarasi wanawake na kupata usajili chini ya sharia ya msajili wa vyama Act Cap,337 R.E 2002 na usajili ulikamilika Novemba 4 2020 chini ya msajili wa vyama wizara ya mambo ya ndani namba S.A 22204.
Alisema ujenzi mungine ni daraja la Mpapa katika barabara ya Mlowo-Kamsamba linalogharimu Tsh,Bilioni 7.365, unaojengwa na kampuni ya Abemulo Contractor ambapo ujenzi bado unaendelea.
Aidha Mhandisi Bishanga alisema ujenzi mungine ni Daraja la Kabalisi katika barabara ya Ibungu-Kafwafwa wilayani Ileje,unaotekelezwa kwa Tsh,Bilioni 7.942 mkandarasi akiwa ni Jassie & Compan limited.
Anaongeza kuwa pia kuna ujenzi wa kingo za kuzuia mmomonyoko wa udogo katika barabara ya Ndembo-Ngana wilayani Ileje uliogharimu Tsh,Bilioni 8.820 unaotekelezwa na mkandarasi Mbuya’s Contractors.
Alisema pia kuna mradi wa barabara ya kiwango cha Lami kutoka Mlowo hadi Kamsamba kwa kuanzia itajengwa kilometa 5 kwa Tsh,Bilioni 8.5 mkandarasi akiwa ni Clask (T) kutoka jijini Mbeya.
Aidha alisema ujenzi mungine wa barabara tya Lami kilometa 5 unaendelea eneo la Mkwajuni kuelekea Saza katika barabara ya Chang’ombe-Mkwajuni –Makongolosi utakaogharimu Tsh,Bilioni 8.5 mkandarasi akiwa Clask (T) Limited ya jijini Mbeya.
MIRADI MIKUBWA ILIYOKAMILIKA.
Mhandisi Bishanga alisema Songwe ina miradi mbalimbali ya Kitaifa,ambapo miradi miwili mikubwa yenye thamani ya Tsh,Bilioni 124 imekamilika ambayo ni barabara ya Mpemba –Isongole hadi mpakani mwa nchi jirani ya Malawi iliyotumia Bilioni 108 na daraja la Kamsamba lililotumia Bilioni 17.
Alisema ujenzi mungine wa barabara za kiwango cha Lami na madaraja ambayo ipo katika hatua za utekelezaji ni 9 yenye Thamani ya Bilioni 152 iliyo chini ya usimamizi wa wakala wa barabara mijini na vijijini Tanroads.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi waishio kando kando mwa barabara hizo kutumia fursa ya kupata ajira za kazi wanazoweza kuzifanya ili kuinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir omary Makame alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu inatambua mchango wa wananwake na ndiyo maana wizara ya ujenzi imetoa kazi za ujenzi kwa kampuni za wanawake.
Alisema hadi sasa kampuni 15 za makandarasi wanawake nchini wamesaini mikataba kwa ajili ya ujenzi na mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa iliyotoa kazi za ujenzi kwa wakandarasi wanne wanawake ambapo jana wamesaini mikataba kwa ajili ya utekelezaji.
Kazi za barabara zinazotengwa kwa ajili ya wanawake ikiwa ni kazi za class VII mpaka V pamoja na Labour based kutoka Tarura na Tanroads,kabla ya kutolewa kazi hizo itatangazwa tenda na kampuni hizo zinashindana kuomba.
- Get link
- X
- Other Apps






Comments
Post a Comment