Kuzinduliwa kwa zahanati ya Kalila kwaleta faraja kwa jamii


Anaclara Ngatunga,Nkasi

Zahanati ya kalila iliyopo katika Kijiji cha kalila Kata ya Kabwe Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ambayo ilianza kujengwa toka mwaka 2024 imezinduliwa na kuanza kutoa huduma rasmi tarehe 21 oktoba 2025.

Zahanati hiyo iliyogharimu kiasi cha shilingi millioni tisini na moja, laki mbili na kumi na nane elfu na miamoja (91,218,100. ),ambazo ni fedha kutoka kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri, pamoja na nguvu za wananchi inayotarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 2500 wa Kijiji cha kalila na maeneo jirani.


Akizindua Zahanati hiyo, Kelvin Nyamonge Tuyi
Mkuu wa seksheni afya (W) amewashukuru wananchi pamoja na serikali kuu na mapato ya ndani chini ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi waliochangia ujenzi wa zahanati hiyo hadi kukamilika na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kuwahudumia wananchi.

“Niwapongeze sana wananchi wa kalila kwa kuja na wazo la ujenzi wa Zahanati na kisha mkachangia Shilingi milioni kumi na saba laki mbili na kumi na nane elfu na miamoja (17,218,100. ), na kutoa nguvu zenu na muda wenu, pia niwapongeze Halmashauri kwa kuunga mkono juhudi za wanachi kwa kuchangia shilingi milion ishirini na nne (24,000,000.) pamoja na kuishukuru Serikali ya awamu Sita Chini Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh. 50,000,000 za umaliziaji wa Zahanati hii pamoja na ongezeko la milioni 25,000,000. Ya vifaa tiba” ameeleza Bw Tuyi.
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imejipanga kukamilisha miradi mingine kutokana na mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu mingine iliyobakia katika halmashauri hiyo.


Kwa upande wake Bi Maria fidelis ambaye ni mwananchi wa Kijiji cha kalila ameishuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuwajengea Zahanati hiyo ambayo imewapunguzia umbali mrefu wa kufuata huduma za afya katika vijiji vingine.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa