WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA JIMBO WAMETAKIWA KUFUATA KANUNI NA MAELEKEZO YA TUME KUEPUSHA MALALAMIKO NA MIGOGORO



Na Israel Mwaisaka,Rukwa

WASIMAMIZI  wa uchaguzi kutoka ngazi ya mikoa na majimbo ya Rukwa na Katavi wameaswa kusoma katiba,sheria,kanuni.taratibu na miongozo mingine ili iwawezeshe kutekeleza vyema majukumu yao yatakayowezesha kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba,2025.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa tume huru ya taifa ya Uchaguzi  (INEC) Magdalena Rwebangira alipokuwa akifungua mafunzo kwa waratibu wa uchaguzi,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ndani ya jimbo yakiwa na lengo la kuwawezesha kuwajibika kwa weredi mkubwa katika mchakato mzima wa uchaguzi.


Alisema kuwa anatambua kuwa zoezi zima kuelekea uchaguzi mkuu ni mchakato mkubwa ,hivyo ni muhimu kufuata katiba,sheria,kanuni na miongozo ikiwa ni pamoja na kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajiri  kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya kikatiba,sheria,kanunu na taratibu zilizowekwa.

Amedai kuwa ni muhimu kwa Wasimamizi hao kujiepusha kuwa sehemu ya chanzo cha migogoro,Malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na Wadau wa uchaguzi  na kuhakikisha wadau wote wa uchaguzi wanashirikishwa ipasavyo katika hatua mbalimbali kama ambavyo tume imekua ikitoa miongozo  mbalimbali ya kufanikisha uchaguzi mkuu kwa mwaka huu wa 2025.

Awali  mkurugenzi msaidizi idara ya usimamizi wa uchaguzi saida Hillary  alidai kuwa mafunzo hayo ambayo yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini yamelenga kuwajengea uwezo wasimamizi hao wa uchaguzi katika kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kama wanavyoelekezwa katika vifungu mbalimbali vya kisheria wanavyoelekezwa na tume huru ya taifa ya uchaguzi.


Hivyo aliwasisitiza kuhakikisha kuwa wanautumia ujuzi  na uzoefu walionao katika mambo mbalimbali na hata katika eneo hilo la uchaguzi katika kuona mchakato mzima wa uchaguzi unakwenda sawa na kuwa tume haitamvumilia mtendaji yeyote atakayezalisha kero na malalamiko yatakayopelekea kuyumbisha jukumu hilol la uchaguzi.

Wasimamizi hao pamoja na watendaji wote wanaohusika na uchaguzi wamekula kiapo cha kutunza siri na kujitoa uanachama  wa vyama vya siasa mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi  wa wilaya ya sumbawanga Lilian Moses Ndelwa

 



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa