Mwanafunzi matatani kwa kumuua mdogo wake wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo




Na Israel Mwaisaka, Nkasi

Jeshi la Polisi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa Samwel Kayoka (16)kwa tuhuma za mauaji baada ya kumuua mdogo wake Jackson Kayoka (14) kwa fimbo walipokuwa wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi mkoani Rukwa SACP Shadrack Masija ni kuwa tukio Hilo limetokea Jana majira ya saa sita mchana katika kijiji cha Mtenga "A" wakati Watoto hao walipokuwa wakicheza kwa kupigana na fimbo na Katika mchezo huo marehemu alipigwa na fimbo kichwani na kudondoka chini.

Alisema kuwa baada ya marehemu kuanguka chini na kupoteza fahamu alichukuliwa na kukimbizwa katika Zahanati ya Mtenga na wakati jitihada za kumpatia matibabu zikiendelea alipoteza maisha.

Kamanda Masija alidai kuwa wao kama jeshi la Polisi kwa sasa wanaendelea kumshikilia Mtoto huyo huku wakiendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio Hilo na kuwa baaba ya hapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Awali afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Romwald Kapele alidai kuwa Watoto hao ni wa familia Moja na kuwa katika Mila ya kabila la Wasukuma ni kawaida kwa kwa Watoto wa umri huo kucheza michezo ya namna hiyo ya kupigana kwa fimbo na kuwa hata baada ya tukio Hilo kutokea mtoto anayetuhumiwa kuwa hakukimbia na badala yake alikua akishangaa tukio lenyewe.

Alidai kuwa baada ya taratibu mbalimbali za Kipolisi kufanyika ndugu walikabidhiwa mwili wa marehemu na taratibu za mazishi zimefanyika Jana.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa