WANANCHI SONGWE WACHEKELEA VIFAA TIBA,WAMTAJA RAIS DKT,SAMIA.
BIIION150 ZA RAIS DKT,SAMIA ZATUMIKA UNUNUZI WA VIFAA TIBA KATIKA UTAWALA WAKE.
MAKALA
Na Ibrahim Yassin,Songwe
‘’uwepo wa vifaaa tiba zikiwemo mashine za kisasa umepunguza msongamano wa wagonjwa kutibiwa kwa waganga wa tiba za jadi,ambao wengi wao walipoteza maisha,Rais Dkt,Samia ametupa matumaini ya kuishi’’.
IMEELEZWA kuwa uwepo wa vifaa tiba zikiwemo mashine za kisasa katika vituo vya kutolea tiba halmashauri ya wilaya ya Songwe kumepu nguza vifo kwa baadhi ya wagonjwa hasa mama wajawazito walioenda kutibiwa kwa waganga wa tiba za kienyeji, Dira kamilifu imeelezwa.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wilayani humo,wakazi wa wilaya hiyo,wameeleza kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na mabore sho makubwa yaliyofanyika kwenye vituo vya kutolea tiba baada ya serikali ya awamu ya sita kufunga mashine za kisasa.
Amos Zakayo mkazi wa Mkwajuni,amesema wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya mpya nchini zilikokuwa zikikabiliwa na upungufu wa vifaa tiba na hata watumishi kwa muda mrefu,akieleza katika awamu ya sita wameshu hudia vifaa tiba vikiwekwa zikiwemo mashine za kisasa.
Safia Mwashilindi mkazi wa Saza,amesema mika ya nyuma walikuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji kupata huduma za matibabu ikiwemo kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma bora na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea tiba lakini awamu ya sita wameondokana na hali hiyo.
‘’Wakati tunajifungua kwa waganga wa tiba za kienyeji,wengi wao walipo teza maisha na wengine walipoteza watoto,tangu aliposhika urais Dkt,Sa mia Suluhu wameondokana na kadhia hiyo kwani kila kituo cha kutolea tiba kina vifaa vya kisasa’’amesema Mwashilindi.
Jumanne Sikanyika mkazi wa Mbangala,amesmea katika awamu ya sita vituo vyote vya kutolea tiba vimeboreshwa kwa kuwekewa vifaa tiba na dawa za kutosha ikiwemo kuongezewa watumishi ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo zahanati moja ilikuwa na wahuduma wawili.
Amesema mbali na serikali kuwapatia vifaa hivyo vya kisasa,pia viongozi waliopo akiwemo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Secilia Kavishe wamekuwa wakifuatilia na kusimamia vizuri hali iliyope lekea uthamani kubwa wa kazi ya serikali kuonekana.
Mganga mkuu (DMO) wilayani Songwe Dkt,Kelvin Mwasha,amesema ni kweli awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu wameweza kupokea vifaa tiba vya Tsh,1500.000.000 vilivyoondoa changamoto ya uhaba wa dawa na mashine za kisasa.
‘’Rais Dkt,Samia amewaheshimisha kwani mbali na kutoa vifaa tiba vya fedha hizo,pia ameboresha huduma zote za matibabu ngazi ya kijiji kata na hata wilayani,wagonjwa wanafika na kutibiwa kwa wakati,pia mkuru genzi Kavishe na timu yake wamekuwa wakitufuiatilia kwa ukaribu kuona utendaji kazi’’amesema Dkt,Mwasha.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Secilia Kavishe,mbali na kukiri mabadiliko makubwa ya uwepo wa vifaa tiba na mashine za kisasa,pia amesema wamepelekewa magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance) zinazobeba wagonjwa wanaopelekwa kutibiwa hospitalini wakitoka kwenye zahanati.
0715869996--0766936392







Comments
Post a Comment