BIL 6.830.ZA RAIS DKT SAMIA ZATUMIKA KUJENGA VITUO VYA KUTOLEA TIBA NA UNUNUZI WA VIFAA.

                        MAKALA

‘’serikali ya awamu ya sita umeondoa vifo vya mama na mtoto,kwa kujenga zahanati kila kijiji,kituo cha afya kila kata na hospital ya wilaya,awali tulitibiwa kwa waganga wa kienyeji na wakunga wa jadi,wengi walipoteza maisha hasa watoto baada ya kuzaliwa’’

Na Ibrahim Yassin,Songwe

MAELFU ya wakazi wa wilaya ya Songwe mkoani hapa,hasa wajawazito waliokuwa wakitegemea kuzalishwa na wakunga wa jadi wamepata matumaini mapya baada ya serikali kujenga hospitali ya kisasa ikiwa na vifaa tiba.

Wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya 5 mkoa wa Songwe yenye post kodi namba 54100, Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 229,219 .

Katika wilaya ya Songwe maeneo maarufu ni Mkwajuni ambako ndio makao makuu ya wilaya. Saza ni eneo maarufu kwa uchimbaji madini na kuna mgodi mkubwa wa Shanta Gold Mine, Kanga na Mbangala.

Ilianzishwa mwaka 2015 ikiwa imepakana na wilaya ya Momba mkoani hapa na Milele mkoani Katavi upande wa chini na upande wa chini imepakana na wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa

Wabungu ni kabila ambalo linapatikana katika wilaya ya Songwe na linachukua asilimia 50 ya wakazi wa wilaya ya hiyo likifuatiwa na Wasukuma, Wanyiha na Wanyamwanga.

Inasadikika kuwa Wabungu asili yao ni Wasagara kutoka Kilosa Morogo ro,ambao walihamia karibu na mlima Kwimba kwa ajili ya tabia yao ya uwindaji,ambapo mpaka sasa wanafanya matambiko yao katika mlima huo.

Wakati wilaya hiyo ikimegwa kutoa wilaya ya Chunya mwaka 2015 kuliku wa na changamoto nyingi za matibabu ambapo kuilikuwa na hospitali moja pekee inayomilikiwa na Kanisa hivyo wakazi wengi waliyimia tiba za kieny eji pindi walipougua.

Shughuri kubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa wilaya hiyo ni uchimbaji wa madini ya dhahabu,ambapo endapo mchimbaji anapata tatizo la kuumia mgodini ililazimika akimbizwe hospitali mkoani Mbeya lakini kwa sasa jambo hilo halipo.

Katika kipindi cha miaka 4 ya Rais Dkt,Samia serikali imefanikiwa kuwatoa wananchi kwenye changamoto ya kutibiwa kwa wakunga wa jadi kwa kujenga zahanati kila kijiji,kituo cha afya kila kata na hospitali ya wilaya.

Sala Mwashilindi mkazi wa Mkwajuni,anasema kabla ya kujengwa vituo vya kutolea tiba yeye ni miungoni mwa watu waliopoteza watoto wakati akitibiwa kwa mkunga wa jadi baada ya kukosa fedha kwenda kujifungulia hospitalini.

Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya wilaya na ujio wa vifaa tiba na mashine za kisasa umewaondoa katika lindi la kujifungulia kwa wakunga wa jadi na kuyaweka maisha yao rehani,kwani kwa sasa wanatibiwa bure na kwa haraka Rais Dkt,Samia akitajwa kuwakomboa.

Ornest Claud mkazi wa Mkwajuni,anasema mafanikio makubwa yaliyopo kwa serikali ya awamu hii ni kufanikisha huduma ya bima ya afya,wakifika hospitalini hakuna foleni wala ubabaishaji wanatibiwa kwa wakati.

Anasema ujenzi wa miradi mipya ya afya umerejesha tabasamu kwa wananchi wa Songwe,kuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt,Samia na serikali yake,vifaa tiba vipo,magari ya kubebea wagonjwa yapo huduma za mama na mtoto ni bure katika hilo serikali imepiga hatua.

George Anthon (ZAZY) mkazi wa Mkwajuni,anasema,miaka mine ya utawala wa Rais Dkt,Samia sekta ya afya imetendewa haki,miradi vituo vingi vimejengwa na wasimamizi wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji secilia Kavishe wamezitendea haki fedha za serikali.

Anasema kabla ya hapo walipata shida hasa wanawake wajawazito na watoto walitozwa fedha kwenye hospitali ya Wamisionary hali iliyowalazimu wengi kukimbilia kwa wakunga wa jadi na wengine walikufa na wengine walipoteza watoto.

‘’Mkurugenzi Kavishe,mwenyekiti wa halmashauri Abraham Sambila,mbunge Philipo Mulugo walitengeneza utatu mtakatifu huku wakishauriwa na kamisaa mkuu wa wilaya Solomon Itunda aliyehamia Mbeya,kwa ushirikiano wao kazi nyingi zilifanyika na kufanikiwa kumaliza migogoro’’anasema.

Mganga mkuu (DMO) wilayani humo,Dkt,Kalvin Mwasha anasema ni kweli awamu ya sita imefanikiwa pakubwa sekta ya afya ,kwani karibu vijiji vyote vina zahanati na kata zote zina vituo vya afya na wilayani imejengwa hospitali ya kisasa.

Anasema Rais Dkt,Samia katika kipindi chake katika sekta ya afya,ameiwezesha wilaya hiyo,fedta Bilioni 6,830,700,000. Zilizotumika kujenga hospitali,umaliziaji wa zahanati na vituo vya afya pamoja na vifaa tiba.

Anasema hospitali ya wilaya imejengwa kwa Tsh,3,630,700,000, vituo vya afya vipo vitano walipokea Tsh,1,500,000,000,Umaliziaji wa zahanati 37 walipokea Tsh,400,000,000 na vifaa tiba walipokea Tsh,1,300,000,000 na kuifanya gharama kuwa Tsh,Bilioni 6,830,700,000 katika utawala wake wa miaka 4.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Secilia Kavishe,anasema mbali na mapokeo ya fedha hizo pia Rais Dkt,Samia aliwawesha magari 3 ya kubebea wagonjwa wakiwemo mama waja wazito wanaohitaji huduma kwenye hospitali ya wilaya.

Anasema magari hayo yanatumika kusafirisha wagonjwa wa dharura ikiwemo wajawazito na watoto kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya wilaya kutoka vijijini na kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kibingwa magari hayo yanawabeba kwenda hospitali ya mkoa nay a rufaa.

Anasema kazi kubwa waliyo nayo ni kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi hiyo ili iwezi kuwasaidia wananchi na vizazi vijavyo kwani serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu.

SHUGHURI ZA KIUCHUMI.

Wabungu wanajishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji mdogo wa Madini na Uhunzi.  Katika kilimo wanalima Mahindi, Mtama, Ulezi na Jamii ya mikunde kama Kunde, Maharage n.k.; Wanafuga ng’ombe, Punda kwa usafiri, Mbuzi, Kondoo.

Wananchi Wanachimba dhahabu kwa teknolojia duni. Wahunzi wanatengeneza zana za matumizi ya nyumbani kama shoka, Nyengo. Vilevile zana za kilimo kama majembe madogo ya kupandia na Silaha kama Mikuki na mishale.

Hivyo kutokana na hali hiyo wanahitaji kuwa na afya njema ndiyo maana serikali imejenga vituo vingi vya kutolea tiba ikiwemo kituo cha dharura hadi ngazi ya vijiji ikiwa na lengo la kulinda afya za wananchi,kuachana na fikra za kizamani.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa