DC_DED WAWAASA VIJANA KUTOKAA VIJIWENI KUPIGA SOGA. WAKITENGA BIL.1.39 ZA MIKOPO.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
VIJANA waaswa kuto kukaa vijiweni kupiga soga na kujadili mambo ya umbea na badala yake wametakiwa waunde vikundi wapate mikopo wajiingize kwenye ujasiliamali.
Kauli hiyo ilitolewa siku za hivi karibuni na mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda akiwa kwenye ziara zake ngazi za vijiji na kata wilayani humo.
Katika ziara hizo Itunda mbali na kukagua miradi ya maendeleo pia aliitisha mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10.
Alisema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu awali ilisitisha utoaji wa mikopo kwa sababu ya changamoto kadhaa lakini tayari imeruhusu mikopo hiyo inayotolewa bila riba.
Alisema wananchi walio kwenye vikundi waendelee kujiimarisha na wasio na vikundi wajiunge watapatiwa elimu na maafisa maendeleo ya jamii kisha wasajiliwe kwa ajili ya kupatiwa mikopo.
" Fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu zipo na tayari baadhi ya vikundi vimeoatiwa, wale wasio na vikundi jiungeni ili mpate mikopo mjikwamue katika lindi la umasikini"alisema.
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Secilia Kavishe katika ziara zake za kupitia miradi ya maendeleo amekuwa akiwaasa vijana kutumia fursa hiyo ya mikopo ili wajiingize kwenye ujasiliamali.
Alisema halmashauri imetenga kiasi cha Tsh, Bilioni 1.39 kwa ajili ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 bila riba kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu lengo kuu ni kumuondoa mwananchi kwenye lindi la umasikini.
Afisa maendeleo ya jamii wilayani Songwe Thomas Kiowi alisema tangu mwezi Novemba 30/2024 jumla ya vikundi 22 vilipatiwa mikopo ya Tsh, Milioni 331,997500 awamu ya kwanza.
Alisema wanaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuunda vikundi ambapo muitikio umekuwa mkubwa kwa wanaohitaji.
Alisema maafisa watendaji,maafisa wengine wakiongozwa na mkurugenzi,mkuu wa wilaya, Mbunge , mwenyekiti wa halmashauri na madiw ani wamefanya kazi kubwa ya hamasa.
Alisema awamu ya pili ya utoaji wa mikopo itatolewa kwenye vikundi vitakavyokidhi vigezo kama ilivyokuwa awali na pia idadi kamili ya vikundi hai itatolewa baada ya zoezi kukamilika.






Comments
Post a Comment