KIJIJI CHA KANAZI KUNUFAIKA NA MAJI YA KISIMA,


Naibu waziri wa Maji Kundo Andrew Mathew jana tarehe Machi,03,2025 amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa katika ziara hiyo Naibu Waziri wa maji pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Mkangale na amekagua mradi wa maji mtaa wa Isunta akiridhishwa na utekelezaji wake.

Kutokana na mradi wa maji uliopo kijiji cha Kanazi kutoanza kutoa huduma ikamlazimu Naibu Waziri wa maji Kundo Mathew kutoa maelekezo ya serikali kuwa siku tano RUWASA mkoa wa Rukwa iwe imekamilisha matengenezo madomadogo ili wananchi wanufaike na matunda ya mradi huo.

Mhadisi BRUNO ISAKWISA Mratibu wa Programu ya visima 900 mkoa wa Rukwa akieleza taarifa ya Mradi huo akisema visima saba (07) vinavyochimbwa katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi ni pamoja na Lyele,kanazi,kipundu,kakoma,Ng*udwe,china na Mnyula na visima hivyo vilivyopata maji vimefikia asilimia 78 huku visima viwili (02) vimekosa maji Kalundi na lunyala .



Kwa upande wao Wakazi hao wa kijiji cha Kanazi wamempokea Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew kwa nderemo na vifijo wakiwa na matumaini ya kuanza kupata huduma ya maji ambapo Wametoa kilio hicho wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Kanazi.

Wakazi wa kijiji cha Kanazi wilaya akiwemo Ludis ulaya na Stela Kwimba wamemuomba Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Andrew Mathew kuharakisha upatikanaji huduma ya maji kwenye mradi wa visima 900 alioweka jiwe la msingi ili kuwapunguzia adha ya wananchi ya kutafta maji zaidi ya kilomita saba (7).


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa