RAIS -DKT,SAMIA AWAFUTA MACHOZI WACHIMBAJI WADOGO AKIWAONDOLEA KERO SUGU
MAKALA
VITALU 19 VYA UCHIMAJI DHAHABU VYALETA UNAFUU WA MAISHA KUPUGUZA VITEDO VYA UHALIFU WILAYANI SONGWE
ZAIDI ya vijana 12,000 kutoka Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe wamepata fursa ya ajira katika migodi ya wachimbaji wadogo na wa kati baada ya Serikali kugawa vitalu 19 kwa wachimbaji huku ikilezwa kuwa vimechochea ukuaji wa uchumi pamoja na kupunguza migogoro na uhalifu katika jamii ya wachimbaji,,anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe.
Wachimbaji wa dogo ni nguzo muhimu katika sekta ya madini wanaoingiza pato kubwa kwenye bajeti ya serikali na kuwezesha vijana kujiajili,lakini licha ya umuhimu huo vijana hao walisahaulika na hata kero zao hazikupata kutatuliwa.
Akizungumza leo Juni 16/2024 mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoa wa kimadini Emmanuel Kamaka anasema upatikanaji wa maeneo ya uchimbaji ilikuwa ni changamoto na kwamba wakati wa utawala wa Hayati Dkt,Magufuli Rais Dkt,Samia akiwa makamu wake alifika wilayani humo kusikiliza kero.
Amesema hata walipoenda Dar es salaam katika mkutano ukumbi wa Mwl Nyerere walijadili upatikanaji wa maeneo ya uchimbaji pamoja na soko la pamoja la kuuzia madini kudhibiti utoroshwaji,wakati huo walikuwa wakichangia asilimia 1 pato la taifa.
Amesema baada ya Rais Dkt,Samia kuingia madarakani wameweza kutatuliwa baadhi ya kero na kufanikisha ujenzi wa masoko ya pamoja hali iliyosababisha serikali kukusanya feha nyingi hata wao kuchangia asilimia 51 pato la Taifa.
Amesema siku za hivi karibumi waziri wa madini Antony Mavunde alifika na aliwapatia vitalu 19 kati ya 35 walivyoomba hali iliyowafu rahisha wachimbaji na kujiona na wao ni sehemu muhimu katika serikali kwani haikuwahi kutokea hali hiyo.
Nae Emmanuel Jimmy,mchimbaji mdogo amesema ana kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt,Samia kwani katika kipindi cha utawala wake miaka 3 ameweza kuipaisha sekta ya madini na hata wao kupatiwa maeneo ya uchimbaji na kuwa madini kwa sasa yanauzwa kwa beielekezi.
Lugangiza Malembo ni afisa madini mkazi mkoani Songwe amesema upatikanaji wa vitalu hivyo 19 vimeongeza chachu ya kujituma kwa wachimbaji wadogo ambao kwa sasa watakopesheka kwa kuwa wamepatiwa leseni.
Amesema miaka mitatu ya Rais Dkt,Samia Suruhu hali ya kipato kimeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma,kwani madini yote yanauzwa kwa bei elekezi ambayo kwa gram 1 Tsh,176,000 na wanunuzi wote wapo sehemu moja serikali inachukua mapato kiurahisi,hakuna utoroshwaji wa madini.
Mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda amesema serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha wachimbaji hao,hivyo vijana watajikita kuchimba na kujiingizia kipato hali itakayoondoa uhalifu.




Comments
Post a Comment