Auawa kwa kuchomwa na moto polisi wahaha kubaini chanzo



Na Ibrahimu Yassin,Songwe

KIJANA mmoja ambaye hajafahamika mara moja, amekutwa ameuawa na mwili wake kutupwa na kuchomwa moto kitongoji cha Mpakani karibu na reli ya TAZARA Kata ya Hasanga,Mbozi mkoani Songwe usiku wa kuamkia leo..

Watu walioshuhudia leo asubuhi kwa kuukuta mwili wamesema kijana huyo ameungua maeneo ya mwili mzima na kwamba upo uwezekano kwamba aliuawa kwanza kabla ya kuchomwa moto.

Diwani wa Kata ya Hasanga  Malick Nzowa amefika eneo la tukio na kuthibitisha tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kisema analaani kitendo cha watu kujichukulia sheria mkononi.

Amesema kitendo cha watu kuchukua sheria mkononi kwa kuua ni kosa na aliyehusika akikamatwa atashitakiwa kwa mauaji."Tumekuwa tukitoa elimu mara kwa mara maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Matukio ya mauaji yamekithiri hivyo bado tunakazi kubwa kuhakikisha tunatoa elimu watu waache vitendo viovu" amesema kamada Senga.

Hata hivyo kamanda Senga alitolea mfano kuwa mtu Ameiba plastiki moja la mahindi akikamatwa anauawa kama kuku. na kwamba sheria zipo wazi mtuhumiwa anatakiwa apelekwe kwenye vyombo husika.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa