MBARONI KWA KUMTUPA MTOTO CHOONI BAADA YA KUJIFUNGUA



Na Israel Mwaisaka,Rukwa

Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Mwanamke mmoja aliyefahamika Kwa jina la Anifa Mwanawima (36) mkazi wa Kijiji Cha Mashete wilayani Nkasi Kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa Rukwa Shadrack Masija ni kuwa tukio Hilo limetokea Jana baada ya kubainika kuwa mtoto mchanga ametupwa chooni kutokana na harufu Kali iliyokuwa ikitokea chooni ambapo Mama mwenye nyumba alitoa taarifa Kwa majirani zake ikiwa ni pamoja na Kwa viongozi wa Kijiji.

Amesema kuwa kufuatia hari hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kilichopo ndani ya choo ni mtoto walitoa taarifa Polisi ambao walishirikiana kuiopoa maiti ya kuchangia huyo kutoka ndani ya choo Huku ikiwa umeharibika na kutoa harufu Kali.

Kamanda Masija amesema kuwa baada ya uchunguzi wa haraka ilibainika kuwa alikuwepo Mwanamke aliyekua mjamzito aliyekua akiishi katika nyumba hiyo lakini walipomtizama hawakuuona tena ujauzito na kumtilia shaka na kukamatwa na katika mahojiano alikiri kuhusika katika tukio Hilo la kumtupa chooni mwanae.

Alidai kuwa Mwanamke huyo siku tatu zilizopita akiwa mjamzito alipata uchungu na kujifungua Kwa Siri Bila ya mtu yeyote kujua na ndipo alipomtumbukiza chooni mtoto huyo na kufariki dunia.

Pia amefafanua kuwa kutokana na uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa mtoto huyo alikua ni wa kiume na amekaa chooni Kwa muda wa siku tatu Toka atupwe chooni na kuwa mwili wake uliharibika sana.

Na amesema kuwa tukio Hilo limetokana na migogoro ya kifamilia ambapo Mwanamke huyo mwenye Watoto watatu alitengana na mumewe na kwenda kupanga chumba kijijini.

Amesema Kwa sasa wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya Hilo na ukikamilika watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa