Mdau wa maendeleo achangia Mil.1 kuvuta maji shuleni na ukarabati wa Bweni
Na Ibrahim Yassin,Songwe
MDAU wa maendeleo mkoani Songwe Ombeni Nanyaro ametoa kiasi cha Ths,Milioni 1 kianzio zinazotumika kuvuta maji ya kukarabati bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe.
Nanyaro ametoa kiasi hicho cha fedha baada ya kufanya ziara kuite mbelea shule hiyo inayomilikiw a na jumuiya ya wazazi (CCM) baada ya kuona wanafunzi wakitembea kilometa 3 hadi mtoni kusaka maji ambayo hata hivyo si safi na salama.
Akizungumza leo mara baada ya kutoa fedha hizo amesema ameona jinsi watoto wanavyo tembea umbali mrefu kusaka ma ji mtoni na kuamua kuwaita mafundi kuvuta maji na kutoa mifuko ya saruji na mchanga kwa ajili ya ukarabati wa bweni.
Nanyaro ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya shule hiyo na pia ni mjumbe wa mkutano mkuu ccm mkoa amesema tayari ameunga nisha maji safi na wanafunzi wameanza kuyatumia.
Mbali na uwekaji wa maji hayo pia amesema mpango uliopo ni kunu nua vitanda na mago doro ikiwemo kulikarabati bweni la wana funzi kwani limechoka na halina hadhi kutumiwa na wanafunzi.
"Ndugu walimu na wanafunzi pamoja na wana ccm mliopo hapa nas hukuru kwa mappkezi mazuri haya niliyo ahidi nitayakamilisha hivi pu nde.nikimaliza ntaweka compute madaras ani na tv kwenye mabweni ili wanafunzi wajisikie wapo nyumbani"amesema.
Hata hivyo alipotembezwa kwenye bweni la shule hiyo amebainishwa halijapigwa sakafu hivyo ametoa mifuko ya sementi na fedha za mchanga ambapo ndani ya wiki hii ukaranati utaanza.
Suma Mwashitete mmoja wa wanafunzi shuleni hapo,licha ya kushu kuru kwa msaada huo,amesema watahepukika na vihatarishi hata vya kufanyiwa ukatili pindi waendapo kuchota maji mtoni na kuwa ukarabati wa bweni utawapa hamasa ya kusoma.
Akizungumza kwaniaba ya wazazi wenzake shuleni hapo Sarafina Nakandonga amesema mjumbe Nanyaro ana moyo wa kipekee na wameshuhudia ameyafanya mengi ndani ya mkoa wa Songwe.
"Nanyaro kila anapokuwa anashilikishwa ni mwepesi kushiliki endapo anakuwa na uwezo na yupo tayari kuacha shughuli zake zote lakini akawa tayari kuwatumikia wananchi na huo ndio uongozi.ametubeba sana hapa mkoani"amesema



Comments
Post a Comment