MKULIMA WA ZAO LA MIHOGO AJITOLEA KUJENGA SHULE INAYOONGOZA KITAIFA KUSAIDIA WENYE UHITAJI.
- Get link
- X
- Other Apps
‘’Mimi nilisomeshwa na Padri Lyaunga wa kanisa la Katoliki kwa sasa ni marehemu alizikwa Lupa tinga tinga,nikaanza kulima hekari 70 nilipopata fedha nikaanza kujenga shule iitwayo Save Life inayoongoza Kitaifa kusaidia wenye uhitaji’’.
Na Ibrahim Yassin,Mbeya
JAMII Nchini yaaswa kujikita katika kusaidia jamii yenye uhitaji hasa katika sekta ya elimu na kilimo ili iondokane na lindi la umasikini na kujikwamua kiuchumi.
Lupi Charles Mwaipalu ni mkazi wa kijiji cha Kandete Kata ya Itope wilayani Kyela mkoani Mbeya,ni mkulima wa zao la mihogo aliyekuwa mfano wa kuigwa kwa kujenga shule ya darasa la awali hadi darasa la saba kusaidia wenye uhitaji..
Wakulima wengi wa Kyela wamekuwa wa hawalipi kipaumbele zao hilo wengi wao wamejikita katika zao la mpunga na Kakao ambao kwa sasa wameanza kujifunza uzoefu kwa mkulima huyo.
Mwandishi wa Makala hii,alifika katika kijiji hicho iliyopo shule ya Save Life (Saidia Maisha) kuzungumza na mkurugenzi huyo ambaye alitoa historia yake kuwa alisomeshwa bure na Pandri Lyaunga na baadaye alisomea uchungaji na kupewa kanisa katika kijijini kwao.
Anasema baada ya kupata uchungaji baba yake mzazi ambaye naye alikuwa mchungaji alikuwa akimiliki mashamba ambapo alianza kulima zao la mihogo huku soko kuu likiwa Sabasaba jijini Dodoma na Mabibo jijini Dar es salaam.
Anaendelea kusema kuwa analima zaidi ya hekali 70 ambapo wateja wanapofika na magari katika mashamba yake anawauzia hekari moja Milioni 2 anapata Milioni 140 kwa mwaka na kila anapovuna fedha hizo anajenga madarasa ambapo kwa sasa yapo madarasa 7 jengo la utawala vyoo na ofisi.
Anasema mwaka 2013/2014 wastani wa ufauru ni 221.1 shule ikiongoza kiwilaya na Kimkoa,ambapo mwaka 2024/2025 wanafunzi walikuwa 16 waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne ambapo wastani wa ufauru ulikuwa 291.7 na kuwa wa kwanza kiwilaya,Kimkoa na kitaifa.
Kutokana na hali kwa sasa yupo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa bweni kwa ajili ya kulaza wanafunzi ambao kwa sasa wanafunzi wapo 390 walimu 20 akiwa na lengo kusajili wanafunzi wengi na kuongeza walimu.
Anasema katika idadi hiyo ya wanafunzi,watoto 14 anawasomesha kwa kuwalipia ada na mahitaji mengine wakilala shuleni hapo huku wengine wakilipa ada rafiki kwa ajili ya uendeshaji wa shule zinazotumika kuwalipa walimu na huduma zingine za msingi.
‘’Ndugu mwandishi nilianza na wanafunzi 3 hadi sasa wapo 390,najivunia shule yangu kuwepo katika shule 10 bora kitaifa,nipo kujenga bweni litakalokamilika mwezi septemba 12 mwaka huu, na nitasajiri wanafunzi wengine na kuongeza walimu’’anasema Mwaipa
Anasema kipato hicho anachopata kila mwaka ameweza kukamilisha majengo yote na kununua mabasi manne yaliyokidhi vigezo vinavyohitajika yanayotumika kubeba wanafunzi kwenye makazi yao kuja shuleni na kuwarudusha.
Aidha Mkurugenzi Mwaipalu anasema alianza kununua ekari 2 za eneo ambapo kwa sasa shule ina ekari 18 huku apande wa chini kukiwa na miti ya asili na ya kimvuli,upande wa juu kuna uwanja wa michezo,bembea na upande wa kushoto kuna mabwawa ya kufugia samaki.
Anasema katika mabwawa amefuga samaki aina ya magege yanayotumik a kwa kitoweo cha wanafunzi,huku upande mungine analima mboga mboga hali inayopelekea watoto kula mlo kamili na kuwaongezea tija na usikivu wawapo darasani.
Meneja wa shule hiyo,Tumaini Mwasanjala anasema anajivunia kuwa mwajiliwa wa shule hiyo,yenye mandhari mazuri ikiwa na mabwawa ya samaki na ng’ombe wa maziwa yanayotumika kwa chakula cha shule.
Anasema pamoja na mambo yote anajisikia faraja shule kuingia katika 10 bora kitaifa huku wakiwa na mipango endelevu kuhakikisha wanakuwa wa kwanza miaka yote kwani mwakani watakuwa na darasa la saba wakijipanga kuhakikisha wote wanapata alama ya kwanza.
Ndigwako Mwamunyange ni mmoja wa wazazi wenye watoto shuleni hapo,anasema walimu wanaitendea haki shule hiyo,kwani watoto wao wanaongea rugha zote huku wakiwa na uelewa mkubwa licha ya kuwa ni wa madarasa ya chini.
Anaeleza kuwa ombi lao ni kuona bweni linakamilika ili watoto wawe wanalala shuleni hapona kwamba wanasubiri kwa hamu kuona wanafu nziwa darasa la sababa mwakani wanapata alama ONE ya ufauru Itakayopelekea wilayaya Kyela kuwa na sifa mara dufu.
''Ndugu mwanahabari,kijana huyu alikuwa na uweza wa kujenga nyumba za kulala wa geni na klabu za kuuzia pombe kama ilivyo kwa vijana wengi,lakini amejenga shule ili kuwakoimboa wana jamii'' anasema Mwamunyange.
- Get link
- X
- Other Apps





Comments
Post a Comment