VITENDO VYA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO VYAPUNGUA NKASI




Na Israel Mwaisaka,Nkasi
‎Uwepo wa maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata,kamati za kupambana na ukatili na uwepo wa asasi za kiraia katika maeneo mengi kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya ukatili katika jamii.
‎Hayo yamebainika Jana kupitia vikao vya MTAKUWWA vilivyoketi katika kata za Majengo, Kirando na Isale vilivyofadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Kituo Cha sheria na ustawi wa jamii Namanyere (SHEUJANA) katika KUPATA tathimini juu ukatili kati ya Wanawake na Watoto.
‎Katika vikao hivyo ilibainika kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto vimekua vikipungua kwa kiasi kikubwa na kuwa Hilo limetokana na uwepo wa maafisa maendeleo ya jamii katika kata nyingi sambamba na ushiriki mkubwa wa asasi za kiraia baada ya jamii kupata elimu ya kutosha juu ya ubaya was vitendo vya ukatili unaotokea katika jamii.


Mkurugenzi wa shirika la Kituo Cha sheria na Ustawi wa jamii Namanyere Godfrey Ntangare amedai kuwa kulingana na mila na desturi za jamii zimekuwa na nafasi ya kutekeleza vitendo vya ukatili lakini elimu inayoendelea na kusimamia na kamati za MTAKUWWA zimesaidia kwa kiasi kikubwa jamii kuelimika na kipelekea vitendo hivyo kupungua.
‎Alisema kuwa vitendo vingi vya ukatili vinatokana na elimu duni waliyonayo jamii lakini kutokana na mikakati ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kwa kushirikiana na serikali kutoa elimu mafanikio yanaonekana Sasa na kuwa kinachotakiwa Sasa Ni kuongeza nguvu ya ziada katika kutoa elimu.



‎MTAKUWWA Ni pango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na kamati za MTAKUWWA Ni moja ya nyenzo muhimu katika kutoa elimu na kukabiliana moja kwa moja dhidi ya vitendo hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya dola

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa