WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA WAPEWA ANGALIZO KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI.
- Get link
- X
- Other Apps
Na Ibrahim Yassin,Songwe
SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi imetoa rai kwa Makampuni 15 ya Makandarasi Wanawake waliopata fursa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 20 katika barabara ya Ruanda - Idiwili Mkoani Songwe kuutekeleza mradi huo ipasavyo kwa ubora, uaminifu na muda uliopangwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Alois Matei wakati akimwakilisha Katibu Mkuu Balozi Mhandisi Aisha Amour katika ufunguzi wa Kongamano la Tano la Makandarasi Wanawake lililofanyika siku za hivi karibuni jijini Dar Es salaam.
“Mafanikio ya mradi huu wa barabara ambao mmepewa na Serikali wa majaribio utafungua milango kwa miradi mingine zaidi ili Makandarasi Wanawake wengine pia wapate fursa hizo”, amesisitiza Mhandisi Matei.
Ameongeza kuwa Serikali imepanua wigo wa thamani ya miradi inayotolewa kwa Makandarasi Wazawa hadi kufikia Bilioni 50 ikiwa ni hatua muhimu ya kuweza kushiriki miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea hapa nchini na kusisitiza kwa Makandarasi Wazawa wote kuzichangamkia fursa za miradi hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Matangenezo ya Barabara kutoka TANROADS, Mhandisi Dkt. Christina Kayoza ameeleza Serikali inaendelea kukuza Makandarasi Wazawa nchini hivyo amewataka Makandarasi Wanawake kuzitumia fursa hizo wanazopata za utekelezaji wa miradi kuzitumia vizuri kwa kudumisha mshikamano ili waweze kufika mbali na pia kama TANROADS itaendelea kushirikiana na Makandarasi hao bega kwa bega.
Naye, Rais wa Chama cha Makandarasi Wanawake Tanzania (TWCA) Mhandisi Judith Odunga ametaja kuwa katika kipindi cha miaka mitano Chama kimepata mafanikio mengi ikiwemo Makandarasi Wanawake kupewa kazi nyingi za ujenzi wa barabara kwa class V hadi VII pamoja na kazi za Labour based kupitia Taasisi za TARURA, TANROADS na nyinginezo.
“Tunaishukuru Serikali kwani kupitia Mawakala wake wa barabara imeendelea kutangaza miradi maalum kwa ajili ya kampuni za wanawake pekee ambapo ushindani unafanyika miongoni mwetu tu”, ameeleza Mhandisi Odunga.
Chama cha Makandarasi Wanawake Tanzania kimesajiliwa kwa lengo la kuwaleta pamoja Wakandarasi Wanawake ili kuwajengea uwezo kupitia mafunzo mbalimbali na kuongeza ufanisi wa biashara zao, kuwa na sauti ya pamoja katika kusimamia utekelezaji wa fursa mbalimbali zinazowahusu Makandarasi Wanawake.
Wakati hatua hiyo ikiendelea jijini Dar es salaam ,jana pia wizara ya ujenzi chini ya wakala wa barabara mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Songwe imetii agizo la Serikali la kuwpatia
wakandarasi wamawake wazawa kujenga barabara za Lami ambapo imetoa tenda ya ujenzi wa kilometa 20 zinazogharimu Tsh,Bilioni 45.447.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika kujenga barabara ya Ruanda-Idiwili yenye thamani ya Bilioni 45.447 yenye kilometa 20 ambapo kilometa 5 zimetolewa kwa wakandarasi wanne watakaojenga kilometa tano tano ambapo jana walisaini mikataba ya utekelezaji wa mradi huo.
Sehemu ya kwanza ya kilometa 5 zitajengwa na mkandarasi wa kampuni ya M/s ULM Investment na HIGO Investment pamoja na TANZHON Limited JV za jijini Dar es salaam kwa kiasi cha Tsh,11,744,575,894.07 ( Bil,11.745).
Sehemu ya pili kilometa 5 zingine zitajengwa na mkandarasi M/s AB Msengi & Hysten & M/s MSETTI Women Contractor JV wa jijini Mbeya kwa gharama ya Tsh,10,485,464,,175.03 (Bil,10.458).
Sehemu ya tatu ya mradi huo kilometa 5 zitajengwa na mkandarasi M/s Ibra Contractors limited,M/s Nail IT Construction Limited na M/s Kimango Engineering Company limited JV wa jijini Dar es Salaam kwa Tsh,12,464,651,295.28 (Bil,12.465.
Sehemu ya nne nayo ni kilometa 5 zitajengwa na mkandarasi M/s JUDEX Contractor Limited,M/s Cyfloa 2020 Company limited na M/s ML Smart Company limited JV za jijini Dar es Salaam kwa gharama ya Tsh,10,752,024,122.83,(Bil,10.
Maida Waziri mkandarasi wa kampuni ya Ibra Contrctor alisema anakila sababu ya kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kukitambua chama cha makandarasi wanawake Tanzania (TWCA) kwa kuwezeshwa kupatiwa miradi.
Alisema baada ya kuona kazi zote za ujenzi wanapewa wakandarasi wanaume walianzisha umoja wa makandarasi wanawake na kupata usajili chini ya sharia ya msajili wa vyama Act Cap,337 R.E 2002 na usajili ulikamilika Novemba 4 2020 chini ya msajili wa vyama wizara ya mambo ya ndani namba S.A 22204.
Hata hivyo alisema wizara ya fedha kupitia PPRA wameweza kuwaongezea kiwango cha Advance Payment Guarantee kutoka asilimia 15 hadi asilimia 30 na kuwa kampuni za wakandarasi wazawa kwa sasa wanaweza kuomba miradi hadi ya Bilioni 50.
Akizungumza mara baada ya kusainiana mkataba huo,meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini mkoani Songwe,Mhandisi Suleiman Bishanga,alisema miradi mingine inayotekelezwa mkoani humo ni ujenzi wa kiwango cha Lami barabara ya Isongole II –Isoko kilometa 52 kwa gharama ya Tsh,Bilioni 74.
Alisema ujenzi mungine ni daraja la Mpapa katika barabara ya Mlowo-Kamsamba linalogharimu Tsh,Bilioni 7.365, unaojengwa na kampuni ya Abemulo Contractor ambapo ujenzi bado unaendelea.
Alisema mradi mungine ni ujenzi wa daraja la Sange katika barabara ya Ibungu-Kafwafwa wilayani Ileje unaogharimu Tsh,Bilioni 7.371 mkandarasi akiwa ni Gemen Engineering Compan,Limited ujenzi ambapo unaendele.
Aidha Mhandisi Bishanga alisema ujenzi mungine ni Daraja la Kabalisi katika barabara ya Ibungu-Kafwafwa wilayani Ileje,unaotekelezwa kwa Tsh,Bilioni 7.942 mkandarasi akiwa ni Jassie & Compan limited.
Anaongeza kuwa pia kuna ujenzi wa kingo za kuzuia mmomonyoko wa udogo katika barabara ya Ndembo-Ngana wilayani Ileje uliogharimu Tsh,Bilioni 8.820 unaotekelezwa na mkandarasi Mbuya’s Contractors.
Alisema pia kuna mradi wa barabara ya kiwango cha Lami kutoka Mlowo hadi Kamsamba kwa kuanzia itajengwa kilometa 5 kwa Tsh,Bilioni 8.5 mkandarasi akiwa ni Clask (T) kutoka jijini Mbeya.
Aidha alisema ujenzi mungine wa barabara tya Lami kilometa 5 unaendelea eneo la Mkwajuni kuelekea Saza katika barabara ya Chang’ombe-Mkwajuni –Makongolosi utakaogharimu Tsh,Bilioni 8.5 mkandarasi akiwa Clask (T) Limited ya jijini Mbeya.
MIRADI MIKUBWA ILIYOKAMILIKA.
Mhandisi Bishanga alisema Songwe ina miradi mbalimbali ya Kitaifa,ambapo miradi miwili mikubwa yenye thamani ya Tsh,Bilioni 124 imekamilika ambayo ni barabara ya Mpemba –Isongole hadi mpakani mwa nchi jirani ya Malawi iliyotumia Bilioni 108 na daraja la Kamsamba lililotumia Bilioni 17.
Alisema ujenzi mungine wa barabara za kiwango cha Lami na madaraja ambayo ipo katika hatua za utekelezaji ni 9 yenye Thamani ya Bilioni 152 iliyo chini ya usimamizi wa wakala wa barabara mijini na vijijini Tanroads.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi waishio kando kando mwa barabara hizo kutumia fursa ya kupata ajira za kazi wanazoweza kuzifanya ili kuinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir omary Makame alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu inatambua mchango wa wananwake na ndiyo maana wizara ya ujenzi imetoa kazi za ujenzi kwa kampuni za wanawake.
Kazi za barabara zinazotengwa kwa ajili ya wanawake ikiwa ni kazi za class VII mpaka V pamoja naLabour based kutoka Tarura na Tanroads,kabla ya kutolewa kazi hizo utangazwa tenda na kampuni hizo zinashindana kuomba.
- Get link
- X
- Other Apps





Comments
Post a Comment