ZAIDI YA BILIONI 4.8 ZATOLEWA KWA WAKAZI 494 KUPISHA MRADI WA KISASA.



Na Ibrahim Yassin,Songwe

WANANCHI zaidi ya 494 wilayani Mbozi mkoani Songwe wameanza kupokea fedha kwa ajili ya malipo ya fidia ya kupisha mradi wa kitaifa wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (Iboya).

Asilimia 70 ya bidhaa  zinazovushwa bandari ya Dar es salaam zinapita kwenye mpaka wa Tunduma,ujenzi wa ikiwemo  njia nne zitahepusha msongamano wa magari naajari na kuongeza tija za kiuchumi.

Akizungumza leo Agost 31/ 2025 Meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amesema wapo kuwapatia cheki za malipo wananchi kupisha mradi.


Anasema kabla ya kuwapatia malipo hayo serikali ilifanya tathimini kwa kuwashirikisha wenyeji wa maeneo hayo ambapo kila mlengwa analipwa kutokana na ukubwa wa eneo husika.

Amesema eneo hilo la Iboya patajengwa mradi mkubwa wa kitaifa cha kisasa cha ukaguzi wa magari yaendayo katika nchi za kusini mwa afrika (Sadc) itakaoendana na njia nne inayotarajiwa kujengwa.

''Lengo la serikali ni kujenga barabara ya njia nne kuhepuka msonga mano,lakini pia patajengwa mradi huo wa pamoja kwani mkoa huu ni lango kuu la nchi za kusini mwa afrika (Sadc) ajira na uchumi zitaon gezeka mara dufu''amesema Bishanga.

Amesema mradi huo unatarajiwa kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo, wilaya na mkoa kwa ujumla kwani serikali ya wamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu imeweka mikakati wezeshi ya kuongeza uchumi.



Fratson Somber kiongozi wa kimila (Chief) wa Ihanda amesema malipo hayo waliyasubiri kwa muda mrefu na mchakato wake umeenda kwaku sua sua lakini leo hii wamefarijika baada ya kupokea cheki za malipo.

Naye Godwin Msukwa amesema wameusubiri mradi huo toka mwaka 2016 huku ikionekana kuwa ni ngonjela,lakini kwa sasa  tayari wamepewa malipo hayo hivyo fedha hizo zitatumika kujenga nyumba maeneo mengine kupisha mradi.

''Tumepewa fedha,tutajenga nyumba za kuishi na za biashara katika maeneo mengine,tunamshukuru Rais Dkt,Samia kwa kuwezesha wananchi wake kupata malipo haya yatakayoongeza uchumi wenye tija''


Serikali imesikia kilio cha wananchi,malipo yanafanyika,hivyo wanufaika wazitumie fedha hizo kujenga nyumba za kuishi na za biashara,badala ya kuzitumia kkufanyia starehe ikiwemo kuongeza wake,(Nyumba ndogo).



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa