UHARIBIFU WA MAZINGIRA BONDE LA ZIWA RUKWA LAHITAJI SEKTA NNE KUNUSURU.
MAKALA
Na Ibrahim Yassin,Songwe
yassin.ibrahimu@yahoo.com 0766936392.
KUKITHIRI kwa uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji katika bonde la ziwa Rukwa kunahitaji ushirikiano wa zaidi ya sekta tatu kudhibiti, limebainika.
Uharibifu huo wa mazingira unafanywa hasa na wafugaji na wachimbaji madini ya dhahabu ambao baadhi yao wamekuwa wakitililisha maji yenye kemikali kwenye mito na wengine wakikata miti ovyo na kuharibu uoto wa asili.
Baada ya mwandishi wa habari hizi kupata taarifa za uharibifu huo,ulifanyika uchunguzi katika bonde la ziwa Rukwa imebainika kuwa sekta zaidi ya tatu zinahitajika ili kunusulu.
Imebainika kuwa uharibifu mkubwa unaofanywa na wachimbaji wa dhahabu katika Bonde hilo unahatarisha kutoweka kwa miti ya asili pamoja na uoto wa asili kwenye vyanzo vya Maji.
Mwandishi alifika katika vyanzo vya mito ya Lupa, Tete, Zila, Kipoka, Mbuzi, Kalungu, Saza, Lwika, Kilinga na Mto Mlamba Ng'ombe ambako shughuli za uchimbaji zinaen delea kwa kasi na kiharibu vyanzo vya maji pamoja na mazingira.
Mito kama Zila, Lwika na Lupa ndiyo yenye samaki lakini kutokana na wachimbaji kufanya shughuli za uchimbaji hadi ndani ya Mto kumepelekea mito hiyo kuondokewa na uoto wa asili pamoja na miti ya asili.
Utafiti umebaini kuwa elimu kwa wachimbaji hao haijaw afikia zaidi ambapo elimu zaidi inahitajika kutolewa na sekta zote ili waweze kutambua umuhimu wa kutu nza mazingira.
Mchimbaji mmoja aliyejitambulisha kwa Jina la Hussein ambaye anafanya shughuli zake katika maeneo ya Saza Wilayani Chunya anasema kuwa suala la Mazingira ni ngu mu kulizingatia kutokana na wao wachimbaji maeneo ambao wanachimba lazima wakate miti, ili wachimbe.
Hussein anesema hata wanapotakiwa kuingia ndani ya shimo ambalo limekuwa refu lazima watumie miti amba yo ni migumu ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.
"Sisi tunaangalia pesa kama ni masuala ya mazingira tukishachimba tunawachia maeneo yao tunasepa zetu" anasema Hussein.
Akizungumzia kuhusu uharibifu wa mazingira katika Bond e hilo Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya ziwa Rukwa Eng. Jac kson Waled anasema suala hilo linahitaji Sekta zote Nne ambazo zinahusika moja kwa moja na uharibifu wa mazin gira kwenye bonde hilo.
Waled anasema sekta ya Madini, Mifugo, Kilimo na Malias iri zinapaswa kuweka mikakati ya pamoja ili kudhibiti uhar ibifu wa mazingira katika bonde hilo ili kurudisha uoto wa asili uliotoweka ikiwemo kingo za mito zilizomeguka.
Anasema tatizo kubwa lililopo ni uwepo wa wachimbaji ambao huchimba hadi ndani ya mto na kwenye vyanzo vya maji licha ya elimu za mara kwa mara wanazopewa lakini kumekuwa na changamoto kuwadhibiti.
Anasema tatizo linalofanya washindwe kuwadhibiti ni kutokana na wachimbaji kuhama hama na kuingia wapya ambao hawajapatiwa elimu,ni bora leseni kwa wachimbaji hao zisitolewe hadi wapatiwe elimu kunusuru uharibifu zaidi.
''licha ya kutoa elimu kwa baadhi ya wananchi walioko kwenye maeneo hayo lakini shida iliyopo ni wachimbaji wageni kuingia kwenye maeneo pasipo pewa elimu hiyo, tukiungana sekta zote tutafanikisha''anasema.
Anaongeza kuwa sasa serikali inawahimiza wachimbaji kupata lesseni za uchimbaji hivyo basi kabla ya kupewa wanapaswa waelezwe umuhimu wa kutunza mazingira.
Ameongeza kuwa baadhi ya wachimbaji wakikosa dhahabu wanageukia kukata miti na kuchoma Mkaa jambo ambalo amesema limechangia kwa kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira.
Anasema kuwa hata wafugaji nao wamekuwa wakichung a Mifugo kwenye vyanzo vya maji na kuharibu uoto wa asili.
Aidha anasema uwepo wa mifugo mingi kwenye vyanzo vya maji kumechangia pia uwepo wa uharibifu wa mazi ngira ambapo mifugo inaingizwa kwenye mito na kusab abisha kingo kubomoka.
Anasema mifugo mingi inachangia kulainisha mchanga au udongo kwenye vyanzo vya maji pia anassma hata mchanga unaochimbwa na wachimbaji mvua zikinyesha unazama kwenye mito hovyo kupunguza urefu wa mto nakupelekea mto kusambaa hovyo.
Aidha anasema kuwa moja ya jitihada wanazozifanya ni kuunda jumuiya za wananchi walioko kwenye maeneo hayo ili kusaidia kutoa elimu kwa wenzao.
Anasema jumuiya hizo zimekuwa zikiwezeshwa kupewa elimu ili nao waweza kufundisha wenzao umuhimu wa kutunza mazingira.
Akizungumzia kuhusu suala hilo Afisa Kilimo Wilaya ya Chunya Cuthbert Mwinuka anasema kuwa elimu imekuwa ikitolewa kwa wakulima isipokuwa tatizo ni mwingiliano baina ya wafugaji na wakulima.
Pia anasema hata wafugaji ni wakulima hivyo nao wamekuwa miongoni mwa wanaoharibu mazingira.
Anasema wanaendelea kuwaelimisha wakulima juu ya umuhimu wa kutunza mazingira.
Kwa upande wake Mwenyekiti mtaafu wa wachimbaji Mkoa wa Songwe Emma nuel Kamaka anasema wachi mbaji wanapewa elimu lakini tatizi ni kwamba lazima baadhi ya vitu watahusika kuviharibu kama miti na mito.
Anasema dhahabu zinapatikana kwenye miamba ya mawe ambayo ni kwenye mapori kunakopatikana miti mingi, hivyo huwezi kuchimba bila kufyeka hiyo miti.
Aidha amesema hata kwenye mito kuna baadhi ya dhaha bu ambazo zinapatikana kwenye maji kama Arruvial Gold ambayo haihutaji gharama kubwa kuchenjuliwa.
Kwa upande wake Afisa Mifugo wa Wilaya ya Chunya Benedict Matogo amesema kuwa wafugaji wamekuwa wakipewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira ndio maana wamepangiwa maeneo yao ya kuchungia mifugo.
Suala la mazingira inahitaji jitihada za pamoja wakiwemo wandishi wa Habari kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira.
Anasema sekta moja haiwezi kukamilisha kuzuia kwa uharibifu wa mazingira hivyo lazima Watu wa Kilimo, Madini, Maliasiri na Mifugo wajizatiti kutoa semina elekezi kwa wananchi.
Uharibifu wa mazingira ni uzoroteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa,maji na udongo na kupotea kwa wanyamapori na maliasili kutumiwa vibaya.
Uharibifu wa mazingira ni moja ya vitisho kumi vilivyoonywa na jopo la juu la vitisho vikuu la umoja wa mataifa Shirika la raslimali ulimwenguni,umoja wa Mataifa wa Mpango wa Mazingira, Umoja wa Mataifa wa Maendeleo na Benki ya Dunia zimetoa ripoti kwa umma kuhusu afya na mazingira duniani tarehe 1 Mei 1998.
Mabadiliko ya mazingira na afya ya binadamu, sehemu maalum katika ripoti hiyo inaeleza jin si magonjwa yana uwezo wa kuzuiwa na vifo vya mapema bado huzidi kuongezeka kwa ida di kubwa. Ikiwa kuna mareke bisho makub wa katika afya ya binadamu mamilioni afya ya bin adamu.
Mamilioni ya watu watakuwa wangeishi kwa muda mrefu,na maisha yenye afya nzuri kuliko awali.
Katika maeneo maskini katika dunia inakadir iwa kuwa mmoja katika watoto watano hawat aishi kuona siku yao ya kuzaliwa ya tano, hasa kwa sababu ya magonjwa yanayohusiana na mazingira.
Watoto Milioni kumi na moja duniani kote hufa kila mwaka, sawa na wakazi wa Norway na Us wisi, wakiunganishwa na hasa kutokana na malaria,shida za kupumua au kuhara- magon jwa ambayo yanaweza kukingwa.
Madhara ya uharibifu wa mazingira
Hili suala huleta madhara makubwa hasa kwa jamii maana huweza kusababisha vifo na hivyo nguvukazi ya taifa hupungua ambapo hukwamisha maendeleo ya taifa na kuleta changamoto kubwa kwa jamii au taifa kwa ujumla.



Comments
Post a Comment