Serikali yamkana Mwalimu aliyewasimamisha Wanafunzi na kuwa siyo maelekekezo ya serikali
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
HALMASHAURI ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imetoa ufafanuzi juu ya tukio la Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Izinga tarafa ya Wapembe Legiucy Martin Kawimbe anayedaiwa kuwafukuza shule Wanafunzi 9 kuwa hayo hayakua maelekezo ya serikali bali ni mgogoro kati ya Walimu na Wazazi uliojitokeza Kijijini hapo uliopelekea Mwalimu mkuu kuwasimamisha shule na kuwataka Wazazi wao wawatafutie shule nyingine na kuwa alienda kinyume na utaratibu na Wanafunzi hao wamerejeshwa shule na hatua za kinidhamu zitachukuliwa pindi uchunguzi unaoendelea utakapokamilika.
Akitoa ufafanuzi juu ya hilo mbele ya Waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nkasi Afraha Hassan amesema kuwa Mapema Leo Kuna taarifa iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Izinga kuwafukuza Wanafunzi 9 kama ni maelekezo ya serikali na kuwa baada ya kulifuatilia Kwa kina suala Hilo walibaini kuwa Mwalimu huyo aliwasimamisha shule Watoto hao baada ya kutokea kutoekewana na Wazazi wao baada ya Walimu hao kukashiwa na kuwataka wawahamishe shule Watoto hao.
Alidai kuwa hatua zilizochukuliwa za haraka ni kuwarejesha shule Watoto hao bila ya masharti yote kwani hatua alizozichukua Mwalimu mkuu wa shule hiyo ni kinyume na utaratibu na wameanzisha uchunguzi wa jambo hilo na kama ikibainika kutenda kosa Hilo hatua stahiki za kinidhamu na uongozi zitachukuliwa kwani kama mgogoro unawahusisha Wazazi na Walimu Watoto hawahusiki Kwa lolote.
Mkurugenzi mtendaji huyo Alidai kuwa katika taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa maelekezo ya kuwafukuza Watoto hao yalitolewa na wizara ya elimu kupitia Kwa mkuu wa wilaya Nkasi hayana ukweli wowote bali ni migogoro yao tu ambapo Wazazi wa Watoto waliokuwa wamesimamishwa walihitilafiana ambapo Wazazi hao waliwarushia matusi Waalimu wa shule hiyo na ndipo mkuu wa shule alipochukua uamuzi wa kuwasimamisha Wanafunzi hao na kutaka Watoto hao wahamishwe shule hiyo waende shule nyingine,kitu ambacho amedai utaratibu huo haukufuata utaratibu wa kisheria na ndiyo maana wametoa amri ya Watoto hao kuwarejesha shuleni mara moja.
Na akadai kuwa serikali itahakikisha Wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine katika Halmashauri ya wilaya Nkasi watasoma bila kubughudhiwa Wala kuingizwa katika migogoro yoyote ya kijamii na kisiasa.
Wanafunzi hao waliorejeshwa shule katika shule hiyo ni Mathias Sweet beth Kabezya wa darasa la (|||),Anakreda Sweet beth Kabezya (|),Grace Boniface Kabezya (lV) Antonio Boniface Kabezya (lV),Venus Boniface Kabezya ((ll) na Clephace Adabeth Kabezya (lV)
Wengine ni Lilian Sweet beth Kaswanya (V), Rosemary Sweetbeth Kaswanya (lll) na Joseph Sweetbeth Kaswanya (Il)
Mwisho

Comments
Post a Comment