Wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi walalamikia Comdomu ya kike kutumika kinyume cha utaratibu




Na Israel Mwaisaka, Rukwa

WADAU wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamedai kuwa kondomu ya kike haitumiki ipasavyo kiasi kwamba Kwa Sasa chuma kilichopo kwenye kondomu hiyo utumika kama bangiri Kwa baadhi ya Wanawake.

Akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Jana mratibu wa asasi ya SEELS Neoni Sanga lidai kuwa licha ya mbinu mbalimbali za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kuendelea kutumia pia Condomu ya kike ni Moja ya nyenzo muhimu sana katika mapambano hayo lakini imekuwa haitumiki ipasavyo ambapo Kwa Sasa chuma chake kilichopo katika Condomu hiyo utumika kama bangiri za za kuvaa mikononi .

Alidai kuwa katika tafiti walizozifanya wamegundua kuwa Wanawake wengi bangiri walizonazo ni chuma kilichokuwa kwenye Condomu hiyo ya kike na kuiomba jamii kuacha kuvaa bangiri hizo Bali Condomu hiyo ya kike itumike sawasawa kwenye matumizi yake katika harakati muhimu za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Pia alisema kuwa Kwa Sasa wao wapo kwenye mpango wa 93/3 Kwa maana ya kuwa Kila eneo kama vile kupunguza kasi ya maambukizi iwe ni asilimia 93, matumizi sahihi ya dawa 93% na matumizi sahihi ya Condomu 93%.

Mratibu wa Ukimwi wa wilaya ( DAK) John Elias alifafanua kuwa mpango wa asilimia 95/3 ndiyo ambao wao wanautarajia kuleta Mapinduzi makubwa kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa Ukimwi lakini kubwa ni kuyadhibiti maambukizi mapya .

Kuhusu hari ya Ukimwi wilayani Nkasi Alidai kuwa maambukizi mapya yameendelea kupungua Kwa Kasi ya kuridhisha.

Alisema kuwa Kwa Sasa wilaya Nkasi Ina Wagonjwa 7110 kati ya hao Wanaume ni 2939 na Wanawake ni 4471 ambao wanapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Makamo mwenyekiti wa Halmashauri Stephen Kayogolo Kwa upande wake alipongeza jitihada zinazofanywa na idara ya afya katika kuona wanahakikisha maambukizi mapya yanapungua lakini Sasa amewataka wajikite zaidi juu ya matumizi ya Condomu hasa ya kike ambayo imeonekana kuwa matumizi yake yapo chini sana ukilinganisha na umadhubuti iliyonayo Condomu hiyo.

Alidai kuwa kitendo Cha Watu kubadilisha matumizi ya Condomu hiyo na kuwa bangiri ni kwamba Bado hawajaielewa vyema Condomu hiyo kama Ina uwezo mkubwa na madhubuti katika kukabiliana na maambukizi mapya ya Ukimwi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa