MCHIMBAJI MDOGO ATOA AJIRA AKIUNGA JITIHADA ZA SERIKALI,ATOA PENDEKEZO.

                         MAKALA



wachimbaji wadogo watoa mapendekezo namna serikali inavyoweza kuongeza kipato kupitia sekta ya madini

Na, Ibrahim yassin,chunya

yassin.ibrahimu@yahoo.com 0718382817.

Mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika halmashauri ya wilaya ya chunya mkoani mbeya,khamis salum kindai ametoa ajira kwa vijana zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali huku akitoa mapendekezo kwa serikali namna ya kuongeza tija ya uzalishaji ikiwemo kuondoa changamoto zilizopo kwa wachimbaji.

sekta ya madini ni moja ya chanzo muhimu ambacho kinaingiza mapato makubwa na kuwatajirisha watu huku serikali ikitegemea mapato kutokana na tozo kutoka katika sekta hiyo.

ikiwa sekta hiyo ni muhimu ambapo serikali ikiweka mikakati mizuri kuongeza mapato iangazie kufanya maboresho kwa wachimbaji ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo pamoja na maeneo ya uchimbaji kwani kwa sasa wengi wao wamekuwa wakichimba kwenye maeneo yenye leseni za watu licha ya kuwa maeneo hayo hawayatumii.

akizungumza na gazeti hili,khamis rajab salum  ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya kindai enterprises anasema yeye alikuwa mjasiliamali na alifanya kazi ya kuchomelea na baadae alijiingiza kwenye uchimbaji miaka 7 iliyopita ambapo hadi sasa amefanikiwa kuajiri vijana zaidi ya 100 wa kada mbalimbali.kupitia kampuni hiyo.

anasema hadi sasa anamiliki migodi 3 na erusheni 1 ya kisasa inayoongoza mkoa mzima,akiwa na planti 2 moja ipo wilaya ya songwe na mbili zikiwa makongolosi chunya, huku akiwa na karasha kubwa la kisasa lenye uwezo wa uwezo wa kusaga mawe tani 3 na nusu kwa saa.



mbali na hilo salum anasema katika jitihada zake ameweza kumiliki skaveta 2 na vijiko (wiloda) 2,tipa 2,gari la kubebea mitambo (rober),trekta 2, akiwa na mitungi 10 ya erusheni ,mitambo ya kuchomelea pamoja na mambo mengine.

anaongeza kuwa kutokana na hali hiyo ya uwekezaji, amekuwa akilipa kodi kwa wakati pamoja na kutoa mishahara kwa wafanyakazi huku akishiriki kikamilifu kwenye shughuri za kijamii katika maeneo yenye miradi na nje ya miradi.

anasema sehemu ya faida anayoipata amekuwa akitoa misaada kwa watoto yatima kwenye vituo vilivyopo mkoani mbeya na katika siku za hivi karibuni ameweza kutoa mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya tsh,milioni 2.1 kwenye ujenzi wa kituo cha afya makongolosi.

pia anasema ametoa ajira kwa vijana wa ndani na nje ya mkoa, amekuwa akitoa michango kwenye nyumba za ibada, misaada kwa watoto yatima wa kituo cha lulu ophance na kituo kingine kilichopo iyunga na kituo cha wazee wasiojiweza jijini mbeya na kwamba kuna ujenzi wa sekondari unaendelea njia ya kwenda mwaoga pia ametoa mifuko 100 ya saruji ya milioni 2.1.

ombi lake kwa serikali kupitia wizara ya madini.

mchimbaji huyo mdogo anasema sekta hiyo ya madini ni muhimu na inachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa ,hivyo ili mafanikio makubwa zaidi yapatikane serikali kupitia wizara ya madini iwape maeneo maalum ya kuchimba wachimbaji wadogo na kuwapatia mikopo.

anasema wachimbaji wadogo wengi hawana migodi,wengi wao zaidi ya 200 walikuwa wakichimba kwenye eneo linalojulikana kwa jina la gepu lakini alijitokeza mtu mmoja amewafukuza akidai eneo hilo ni lake na amepewa leseni.

kufukuzwa kwa wachimbaji hao kumeongeza mgongano ambapo wengi wao wamekimbilia kwenye eneo lake wakichimba na kuwa hadi sasa makarasha zaidi ya 14 yamefungwa na kila karasha moja linawatu 10 hadi 12 wanaofanya kazi hapo.

‘’ndugu mwandishi,wachimbaji hawa wamefukuzwa kwenye eneo lile la gepu,wamekuja kuchimba kwenye eneo langu na wamefunga makarasha,siwezi kuwafukuza kwa kuwa wanatafuta riziki ila inatakiwa serikali itafute eneo lingine lisilotumika kuwahamishia mwachimbaji hawa ili kuhepuka kutofanyika kwa mambo mabaya ikiwemo wizi.’’anasema.



kindai amesema serikali inapaswa kutambua kuwa wachimbaji ambao hawana maeneo ya kuchimba ndio wazalishaji wakubwa wa dhahabu nchini kwani wao wanapoingia nakujipat ia liziki yao ile ndogo ndiyo huongeza uwingi wa dhahabu kwa mkoa au taifa kwa ujumla.

kindai ameongeza kuwa mbali na kuzalisha ajira lakini pia amekuwa akipokea tuzo mbalimbali kutokana nautendaji wake mkubwa ikiwa ni pamoja na michango yake kwa serikali kama ulipaji mzuri wa matumizi ya umeme ambapo tanesco imempatia tuzo.

amesema kuwa hata ofisi ya madini ilishamutunuku na tuzo kutokana na uzalishaji mzuri wa dhahabu pamoja na uwepo wa mitambo bora ya uchenjiaji wa dhahabu na tuzo nyingine jambo ambalo limepelekea kuwa kampuni bora kwa mkoa wa mbeya.

ameongeza kuwa wawekezaji wengi ambao wanamiliki maeneo makubwa wilayani humo hawana mda wakuchimba lakini wale wenye nia ya kuchi mba na kuzalisha kipato kwa taifa hawapewi kipaumbele cha kupatiwa maeneo ya uchimbaji huku wasiokuwa na njaa ya uchimbaji wakiendelea kuhodhi maeneo.

nae injinia zebedayo mumusi ambaye ni mchimbaji mdogo,anasema kitendo cha vitalu kupewa wachimbaji wenye majina huku wasiofahamika wakikosa hakiwezi kusaidia na kuwa ili usawa wa mgao ufanyike ni bora wahusika wawe wanaitisha mikutano ya hadhara kuzungumzia hadharani ili kila mtu ajue.

“tunasikia kuwa kuna vitalu vimepatikana lakini serikali inapaswa kutangaza au kuitisha mkutano kwenye maeneo husika ili kila mmoja asikie na kama atapenda kupata eneo lake basi iwe ni suala la kuomba lakini wakiwa wame fahamishwa” anasema zebedayo.

ameongeza kuwa hata eneo ambalo lilikuwa hifadhi ya taifa la mbiwe waliopata maeneo hayo ni wajanja ambapo wachimbaji wadogo ambao ndio wazalishaji wakubwa walipaswa kujulisha na sio kufanya mambo kwa kisirisiri.

aidha amesema kama serikali inaona pengine vijana ambao hawana lesseni au hawana uwezo wakupata lesseni kushindwa kumudu gharama za lesseni wangetafuta njia ya kuwapatia kwa vikundi ili hata uwezeshwaji iwe lahisi pia kwani hao ndo wazalishaji wa dhahabu inayochangia kwa asilimia 53 kwa pato la taifa.

amesisitiza kuwa elimu zaidi kwa wachimbaji ifanyike ikiwemo ya kishe ria,kwani migogoro imekuwa ikijitokeza ya wachimbaji na wenye maeneo huku maeneo mengi yakiwa yametelekezwa huku serikali ikiwa inakosa mapato huku akieleza elimu zaidi kwa wauzaji baruti ifanyike kwa wana otembeza kwa kutumia baiskeli.

kwa upande wake george kasanda yeye ni mchimbaji mkongwe kwa sasa anamiliki mgodi na anawafanyakazi zaidi ya 50 huku akitumia uchimbaji wa kutumia mashine zaidi na kwamba wakati wa profesa sospeter muhongo alishika nyadhifa kubwa kwenye shirika la madini na kufanya utetezi kwa wachimbaji wadogo.

anasema wakati profesa sospeter muhongo ni waziri wa madini mwaka 2010  yeye alishiriki kwenye sera ya madini ya mwaka 2010 pale nyumbani hotel jijini mwanza mwenyekiti wa rasimu ya katiba kutoka wizara ya madi ni akiwa nayopa na kwa upande wa miningi filbert rweyemamu akisaidiwa na assa mwaipopo.

anasema ili kuondoa migogoro wataalamu wa wakulima na wachimbaji  waje na vifaa gst na ramani ya mikondo ya madini wawaletee wachimba ji,watoe elimu ya uchimbaji maeneo yenye madini mengi yamewekwa kuwa makazi ya watu kitu ambacho kinawakosesha mapato wachimbaji na serikali kwa ujumla.

anasema uwepo mpango kuwa maeneo yenye mikondo ya madini kusiwe na makazi ya watu na watu wa gst wanapaswa kuwa na ramani na serikali iruhusu watu binafsi kufanya tafiti kuongeza ushindani na kuikuza sekta hiyo.ikiwa ni pamoja na kuelimishwa juu ya usalama migodini.

aidha ameshauri kuwa serikali itafute mitambo ya utafiti ikiwezekana iwakodishie wachimbaji wadogo ili kuendana na technolojia ya kisasa ambapo wachimbaji wengi wanatumia nyezo za kizamani jambo ambalo linachelewesha upatikanaji wa dhahabu kwa wingi.



anasema mitambo ya utafiti ikiwekwa jirani na wachimbaji ni lazima wachimbaji wadogo watakuwa na uwezo wa kukodi badala ya wao kununua kwani kwa sasa gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa lakini kupitia serikali kuwawezesha fifaa vya utafiti suala la kupata kilo zaidi ya 500 kwa mwezi inawezekana kwa mkoa wa mbeya.

waeleza jinsi walivyonufaika kupitia mgodi wa kindai.

ejid kasyani,kutoka geita  anasema kupitia mgodi wa kindai amefanya kazi miaka 7 amefanikiwa kujenga makarasha yake na kuanza uchimbaji,amejeng a nyumba bora ya kuishi,na kufungua taasisi za kifedha na ameajiri na kwam ba anaomba serikali itatue changamoto zinazowakumba wachimbaji wadogo kuongeza tija.

nae samson elisha akisema amefanya kazi ya usimamizi mgodini miaka 6,ameweza kununua viwanja amejenga nyumba na kuendeleza miradi yake binafsi huku gelvas kapange akisema ndani ya miaka 4 kazini ameweza kujenga nyumba na kusomesha wadogo zake,kuboresha makazi ya wazazi wake.

amesema ili kampuni ya kindai ifanikiwe zaidi serikali imuwezeshe afunge mtambo wa cap na kufanya tafiti za miamba kubaini dhahabu ilipo katika vitalu vyake, ambapo peter daud afisa masoko,anasema amefanikisha kujenga mahusiano baina ya wachimbaji na uongozi na hata serikali huku akijifunza zaidi teknolojia ya uchimbaji.

daud anasema kwa sasa ameweza kufungua biashara zake kupitia mshahara aliokuwa akiupata huku akishauri serikali ijenge imani na wachimbaji wadogo,kwa kuwapatia maeneo na mikopo,kuwawezesha mitambo ama vipimo vya madini kuongeza tija.

giveness wikedzi kutoka iringa anasema yeye ni ajira mpya amejipanga kufanya kazi kwa bidii na kupitia mshahara atakaokuwa anaupata atafanya mambo makubwa ya kimaendeleo,huku amina maero toka mwanza anasema kwenye sekta ya masoko atahakikisha bidhaa za kampuni hiyo zinajulikana.

nae tengano mwankusye mkazi wa tukuyu,anasema amefanya kazi miaka 5  kwenye kampuni hiyo iliyoanza na mitungi 3 hadi sasa inazaidi ya mitungi 10 ya elusheni, amejenga nyumba 3 na kununua viwanja 2 huku akinunua mashamba 3yenye ekari 3 kwa kila shamba,amefungua duka la kuuza spea za pikipiki .

mkuu wa wilaya afisa madini waeleza mikakati kuipasisha sekta hiyo.

afisa madini mkaazi mkoani mbeya laulent mayala anasema serikali imejipanga kuhakik isha wachimbaji wanaondolewa chanagamoto zao ikiwa ni pamoja na kupatiwa maeneo ambapo tayari zaidi ya vitalu vyenye leseni 1500 vilivyokuwa havitumiki wamepewa wachimbaji wadogo huku mambo mengine yakiendelea kutatuliwa.

mkuu wa wilaya ya chunya mbaraka batenga anasema kutokana na kuwa sekta hiyo ya madini kuwa na umuhimu,serikali imejipanga kuwaongezea tija wachimbaji na kuweka lengo la kukusanya kilo 500 kila mwezi kwa kufanikisha hilo tayari vitalu vyenye leseni 1505 vilivyokuwa havitumiki vimechukuliwa na kupewa wachimbaji wadogo kwa kuanzia.

mkuu huyo anasema uongozi wake unaendelea kuzishawishi benki ili ziweze kuwakopesha wachimbaji wadogo kwa ajili ya kufanikisha shughuli za uchimbaji kwani anatambua umuhimu wa wachimbaji wadogo na kusema kuwa iwapo benki ikawaamini wachimbaji wadogo anamatumaini kuwa hawawezi kumuangusha kwa kukosa kurudisha mikopo.

batenga amesema hakuna mchimbaji mwenye lesseni ameweza kulalamika kuhusu mchimbaji mdogo kushindwa kurudisha deni hivyo anamatumani kuwa hata benki zikiwakopesha wachimbaji wadogo lazima watatekeleza ahadi zao.

ili kufanikisha na kuipaisha sekta ya madini nchini ipo haja serikali kuwapatia wachimbaji maeneo zaidi yenye madini ya  kuchimba na kuwafanikisha upatikanaji wa mikopo ya fedha na vifaa vya uchimbaji ikiwemo vipimo vya utambuzi wa madini,kwa kufanya hivyo serikali itaongeza mapato mara dufu na wachimbaji watanufaika.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa